Jinsi ya kuepuka uzito mkubwa kwa wafanyakazi wa ofisini

Asilimia kubwa ya ajira siku hizi ni za ofisini na mara nyingi huhusisha kukaa na matumizi ya kompyuta kwa muda mrefu. Wafanyakazi wa aina hii wako katika  hatari kubwa ya kuwa na uzito mkubwa na hata magonjwa kama kisukari na shinikizo la damu. Na mara nyingi hukaa kwa masaa nane hadi tisa kwa wakifanya kazi,hii huongeza hatari yao katika afya zao kama ilivyotajwa hapo awali.

Ila uzito mkubwa na hayo magonjwa ambatanishi vinaweza kuepukika kwa ambao bado hawajapata matatizo hayo na kwa ambao tayari wameongeza uzito wao kwa kiasi fulani.

Yafuatayo ni baadhi ya mambo unaweza fanya ;

1.Jenga tabia ya kwenda n chakula chako ofisini,hii itakuepusha kununua vyakula visivyo na afya kama fast foods mara unapokuwa ofisini na hapa hakikisha kubeba vyakula vyenye afya kama matunda,mbogamboga na vyakula vyenye protini.

2.kunywa maji ya kutosha ,mara nyingine kiu pia kinaweza hisiwa kama njaa hivyo unapokunywa maji unaepusha kula vitu kama chocolate,chipsi au hata soda. Hii pia itakupa nafasi ya kutembea walau kutoka kwenye dawati lako la kazi mpaka sehemu ya maji.

3.kuna matatizo mengi hutokana na kukaa muda mrefu hivyo jiwekee ratiba ya kutembea kidogo kila baada ya angalau saa moja,unawea kufanikisha hii kwa kuweka alarm kwenye simu

4.jijengee tabia ya kutembea na kuhesabu hatua zako hata kwa kutumia app ya simu kama “pedometer” unaweza kuongeza hatua kwa kutumia ngazi badala ya lifti,kupeleka ujumbe kwa mfanyakazi mwenzio ndani ya ofisi badala ya kumtumia ujumbe au hata kwa kupaki gari yako mbali kidogo na ofisi.

5.wakati wa chakula cha mchana toka kwenda kwenye mgahawa kwa kutembea badala ya kuletewa au kutumia gari.

6.unaweza pia ukatumia usafiri wa kawaida kwenda ofisini badala ya gari binafsi hii itakusaidia kuwa na heshima na muda na hat akutumia nguvu zaidi ili kuwahi.

Zaidi ya yote hii inapaswa kuwa tabia yako ya kila siku hata ukiwa nje ya ofisi unatakiwa kula vizuri na kufanya mazoezi walau mara mbili kwa wiki.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show