Jinsi ya kutunza meno bandia ya kuvaa na kuvua (removable denture)

Meno bandia ni mbadala wa meno asilia. Meno haya huweza kuwa ya kuvaa na kuvua (removable denture) ambapo mtumiaji ana uwezo wa kuyavaa na kuyavua bila kuhitaji msaada wa daktari wa kinywa na meno.

Meno bandia yanahitaji matunzo na kufuata masharti ili yaweze kudumu kwa muda mrefu na pia ili kuzuia matatizo yatokanayo na uvaaji usio sahihi  wa meno bandia (ill-fitting denture). Yafuatayo  ni masharti (maelekezo) ya jinsi ya kutunza meno bandia ya kuvaa na kuvua.

  • Usitumie meno bandia ya kuvaa na kuvua kutafunia vitu vigumu kama mifupa.
  • Hakikisha unavua meno yako kila siku angalau masaa 8.
  • Mara unapovua meno hakikisha unayaweka sehemu yenye usalama katika chombo (kopo) chenye maji.
  • Unapovua meno ya bandia tumia kidole au mswaki kusugua taratibu (massage) sehemu ya fizi ambapo meno hayo hukaa ili kuruhusu damu kupita vizuri sehemu hizo.
  • Yasafishe meno bandia kwa maji na sabuni kila siku.
  • Ikiwa ni mara ya kwanza kutumia meno bandia unaweza kupata shida ya kutamka maneno machache,usijali kwani hali hiyo itaisha baada ya kuzoea.
  • Unaweza kuhisi ongezeko la mate mdomoni mara ya kwanza kutumia meno bandia, usijali kwani hali hiyo ni ya muda tu.
  • Ikitokea unashindwa kuvaa meno bandia kwa sababu yoyote ile hakikisha unamuona daktari wa meno kwa uchunguzi na maelezo zaidi.
  • Iwapo meno yako yakivunjika au kupata hitilafu yoyote, muone daktari wa meno kwa ajili ya marekebisho.

Je unatambua kuwa jinsi ambavyo unatabasamu hutegemea hasa meno yako? Naam, ikiwa unajali tabasamu lako utayatunza meno yako kwa kuyasafisha mara mbili kwa siku na kupunguza ulaji wa vyakula vyenye sukari nyingi.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show