Kuchanika kwa kondo la uzazi baada ya wiki 28 za ujauzito (abruptio placenta)

Kuchanika kwa kondo la nyuma la uzazi baada ya wiki ya 28 ya ujauzito.(Abruptio placenta)

Hali hii inatokana na kutengana kati ya kondo la uzazi na tumbi la uzazi kuanzia wiki ya 28 ya ujauzito ambayo husababisha mjamzito kutokwa na damu ukeni.

 

Chanzo cha tatizo

1. Shinikizo la damu wakati wa ujauzito na kifafa cha mimba

2. Mimba ya mapacha

3. Kuumia au kujeruhiwa kwa kondo la uzazi

4. Uvutaji wa sigara kwa wajawazito

5. Kupata tatizo hili kwa mara ya kwanza

6. Matumizi ya madawa ya kulevya

7. Kuwa na maji mengi kwenye tumbo la uzazi

8. Maambukizi katika njia ya uzazi na mji wa mimba

 

Dalili za ugonjwa

1. Kutokwa damu nyeusi au mabonge ya damu ukeni wakati wa ujauzito

2. Maumivu makali ya tumbo

3.Tumbo la uzazi kuwa kubwa

4. Mtoto kutokuwa na mapigo ya moyo ya kawaida

5. Maumivu sehemu ya chini ya tumbo la uzazi wakati wa uchunguzi wa mama

 

Nifanye nini nionapo dalili hizi.

Hali hii hutibiwa kama dharura kwani isipowahiwa ina madhara makubwa sana kwa mama na mtoto ambapo wote wanaweza kupoteza maisha kutokana na upungufu mkubwa wa damu atakaokuwa nao mama mjamzito, hivyo mara moja bila kuchelewa

– mama apelekwe hospitali mara moja kwa uchunguzi na matibabu bila kuchelewa

– matibabu ya kumaliza tatizo ni pamoja na kufanya upasuaji wa dharura ili kuokoa maisha ya mtoto kama bado yu hai

– kumzalisha mama kwa njia ya kawaida kama mtoto amefia tumboni

 

  • Mwisho sio kila damu inayotoka sehemu za siri wakati wa wiki 28 na kuendelea itakuwa ni kutokana na kuchanika kwa kondo la uzazi la nyuma hivyo lazima mama amuone daktari ksa uchunguzi zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show