Nianze lini kuhudhuria kliniki?

 

Takwimu zinaonyesha asilimia 64 tu ya wajawazito huhudhuria kliniki”

Nianze lini kuhudhuria kliniki?

Wamama wajawazito wengi hupata shida kuamua lini hasa waanze kuhudhuria kliniki. Wataalamu wanashauri wakina mama wajawazito wasio na tatizo lolote kuanza kliniki kuanzia wiki ya 10 mpaka 16 hivyo wawe wametembelea kliniki mara zisizopungua 4 katika kipindi cha ujauzito wao.

Takwimu zinaonyesha kuwa wajawazito wachache sana ambao wanawahi kuhudhuria  kliniki hupata shida wakati wa ujauzito na pindi wanapojifungua ukilinganisha na wajawazito ambao huchelewa au hawahudhurii kliniki kabisa.

Kwanini nihudhurie kliniki mapema?

•Kuhudhuria kliniki hukuweka karibu na madaktari hivyo kuhakikisha afya ya mama na mtoto tumboni ipo salama.

•Husaidia kujua na kutibu mapema matatizo ambayo yanaweza kuathiri afya ya mama na mtoto wakati wa ujauzito.

•Unapohudhuria kliniki unapata elimu juu ya uzazi na mabadiliko yanayoambatana na uzazi.

•Kuhudhuria kliniki humuandaa mama kwa ajili ya kujifungua(leba), kunyonyesha na jinsi ya kumlea mtoto.

Hakikisha:-

~Kila uendapo kliniki unapewa tarehe ya kurudi tena na iandikwe kwenye kadi yako.

 Mama mjamzito, hakikisha unahudhuria kliniki mapema katika wakati tajwa ili uweze kuendeleza safari yako ya kuitwa mama vizuri mpaka pale utakapojifungua.

2 thoughts on “Nianze lini kuhudhuria kliniki?

 1. Jaribuni kuelezea kwa undani zaidi maana, mnaelezea kifupi sana. Unaposema mama takwimu zinaonyesha kua wamama wanaowahi kliniki wanapata shida wakati wa kliniki na wakati wa kujifungua, kivipi?

  Huwa tunashauri mama anapo jihisi ni mjamziti aende kliniki, kwani kuna mambo mengi ya kuchunguza na kuyafanyia kazi mapema sana kabla mimba haiyawa kubwa.
  Mfano: amekuja na wk 16 alafu ni HIV positive alafu hajui hali yake. Unategemea nini kwa kiifant?
  Mfano 2; amekuja na wiki 16, ana HB ya 5g/dl unafanyaje?

  Kwahiyo tunashauri sana mama aje klini mapema sana chini ya wiki 12 awe amekuja.

  Reffer to FANC.

  1. Ahsante kwa ushauri, Tunachojaribu kufanya ni kuweka lugha iliyorahisishwa na post moja haiwezi kuelezea kila kitu ndio maana ukiangalia post nyingine utaona kwamba kuna kipande kimoja kimoja kimeelezewa na tutaendelea kuelezea haijaishia hapo.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show