Umuhimu wa kutenganisha mimba moja na nyingine.

Wataalamu hushauri mama mjamzito baada ya kujifungua akae takribani muda wa kama miaka miwili kabla hajapata mimba nyingine tena.

Je,kuna umuhimu wowote wa kufuata maelekezo haya?

Ndio, ushauri huu ni wa muhimu kwa sababu zifuatazo.
• Muda huu humpa mama nafasi ya kurudia hali yake ya kawaida kabla ya kupata mimba nyingine. Mwili wa mama hupoteza virutubisho muhimu kama vile madini ya chuma. Hivyo kupata mimba mapema sana, mama huanza ujauzito akiwa na na virutubisho vilivyo chini sana na humpa mama hatari kama upungufu wa damu.

Kupata mimba zinazofuatana sana pia humuhatarisha mtoto na husababisha madhara kama vile
•Kujifungua watoto kabla ya wakati,hali ambayo humuweka mtoto katika hatari kama maambukizi yanayoweza kuleta afya dhaifu kwa mtoto.
• Mtoto kufia tumboni
• Matatizo wakati wa kujifungua, kujifungua ni tukio ambalo huitaji mwili wa mama kuwa katika hali nzuri kiafya. Kubananisha watoto hufanya mama kuchoka na kushindwa kuhimili tukio zima la kujifungua.
• Mbali na hapo, muda huu humpa mama nafasi ya kulea mtoto wake aliyejifungua tayari kuhakikisha anakua vyema. Ni wakati ambao mama anaweza kutoa muda wake kumlea mtoto badala ya kulea kichanga na mimba nyingine.

Mbali na sababu za kiafya, kutenganisha watoto kunasaidia kujenga familia kiuchumi kuwezesha watoto wote kupata mahitaji muhimu. Wazazi pia hupata muda wa kutosha kwa ajili ya watoto wao.

Kupangilia uzazi kwa idadi ya watoto na muda wa kutenganisha watoto kuboresha afya ya mama na watoto, na kujenga familia bora.

1 thought on “Umuhimu wa kutenganisha mimba moja na nyingine.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show