Maumivu ya maungio ya mifupa na misuli (Osteoarthritis)

Maumivu haya hutokea kwenye mifupa ambayo ipo katika sehemu za maungio ya mwili kati ya mfupa na mfupa. Yamezoeleka kwa kiasi kikubwa kuathiri maungio ya magoti. Watu wengi huchanganya tatizo hili na ugonjwa uitwao gauti (Gout) ambao huathiri maungio ya dole gumba kwenye miguu.

Ugonjwa huu hutokana na uathiri wa fluidi iitwayo sainovio (synovial fluid) ambayo hupatikana katikati ya mifupa miwili iliyopo sehemu ya maungio. Fluidi hii husaidia kuondoa msuguano kati ya mifupa miwili na inapokua inalika kwasababu mbali mbali hufanya mifupa ya sehemu ya kiungio kukutana, na misuguo kati ya mifupa hiyo miwili hutokea na kusababisha maumivu makali sana.

Nini husababisha?

 • Umri: wazee na watu walio na umri zaidi ya miaka zaidi ya 40 (arobaini) ndio waliokua katika hatari ya kuupata ugonjwa huu.
 • Uzito mkubwa: mtu ambae ana uzito wa kupitiliza (obesity) anakua katika hatari ya kuupata ugonjwa huu hata akiwa katika umri mdogo.
 • Kuumia kwenye viungio: ajali, kudondoka au kuumia kwa aina yoyote ambapo pata athiri maungio hayo hupelekea mtu huyo kua na athari ya kupata tatizo hili.
 • Kuvimba kwa magoti (inflammation): ikitokea sababu zinazoweza kupelekea kuvimba kwa magoti humuweka mtu kuwa katika hatari ya kuupata ugonjwa huu.
 • Kurithi (genetics): inapogundulika kua mtu aliye chini ya miaka 40 (arobaini) ana tatizo hili, basi kuna asimilia kubwa kua kapata hili tatizo kwa kurithi katika koo na familia yao.
 • Sababu nyingine ni kama; kufanyisha kazi kupitiliza maungio hayo (mechanical stress), matatizo ya neva na kadhalika.

Dalili zake ni zipi?

 • Maumivu katika viungio vya mifupa. Maumivu hayo huwa kama yanachoma (kama panawaka moto) na ni makali.
 • Maungio kuwa na hali ya uvimbe unapopashika.
 • Maungio huwa na maumivu pale ambapo unajaribu kusogea. Dalili hii hutokea asubuhi kwa muda wa lisaa (huutofautisha ugonjwa huu na magonjwa mengine ya maungio) na pia maumivu baada ya muda mrefu wa kutokufanya kazi yoyote.
 • Uzito wa kuzungusha sehemu ya maungio hayo (inflexibility).
 • Pale utumiapo maungio hayo, unahisi kama kuna msuguano (kusagika) kati ya mifupa.
 • Kutengeneza mfumo wa mfupa mwingine au sehemu ya ungio huwa kama panaongezeka.

Nifanye nini nionapo dalili hizi?

 • Kumuona daktari mara tuu anapo hisi dalili hizi.
 • Hutibiwa kulingana na ukubwa wa tatizo hilo. Dawa kwa ajili ya kupunguza maumivu na uvimbe huweza kutumika.
 • Mazoezi kwa ajili ya kupunguza uzito hushauriwa
 • Vyakula kama nyama na pombe havishauriwi.
 • Kutembea na kufanyisha maungio, mazoezi mepesi pia ni njia ya kupunguza dalili hizi.
 • Haishauriwi pia kubadilisha hali ya hewa kwa ghafla.

Watu wenye tatizo hili hupaswa kua na mpango wa kina dhidi ya kujikimu na tatizo hili. Kuishi maisha ya mazoezi, kutumia dawa zao na ulaji mzuri ni njia moja wapo itakayoweza kuwasaidia kujikimu.

2 thoughts on “Maumivu ya maungio ya mifupa na misuli (Osteoarthritis)

 1. Asante dokta,kuna mahali umesema ugonjwa huu upo tofauti na gauti sasa mimi ningependekeza mtuandalie makala ya gauti kabisa ili tujue tofauti kwa undani,,,hongereni kwa kazi nzuri.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show