Je ni kweli mawe kwenye figo husababishwa na kutokunywa maji tu?

Tatizo la kutengeneza mawe kwenye mfumo wa mkojo hukumba kama asilimia 5% ya watu duniani na hutokea mara mbili Zaidi kwa wanaume ukilinganisha na wanawake. Hatari ya kutengeneza jiwe katika mfumo wa mkojo katika kipindi cha maisha yako ni kama asilimia 8-10. Na hatari ya kujirudia kutengeneza jiwe la pili baada ya kupata shida mara ya kwanza ni hadi asilimia 50.

Figo hufanya kazi muhimu ya kuchuja kemikali katika mzunguko wa damu. Baadhi ya hizi kemikali ni matokeo ya kimetaboliki ya vyakula tunavyo kula, matokeo ya kimetaboliki ya dawa anazotumia mtu na matokeo ya kimetaboliki pale mtu anapo kua na maambukizi ya wadudu aina Fulani.

AINA ZA MAWE
Kuna mawe ya aina 4; mawe ya calcium, mawe ya uric acid, mawe ya struvite na mawe ya cysteine.

KWANINI MTU ATENGENEZE MAWE?
Sababu au hatari ya kutenegeza jiwe hutofautiana na aina ya jiwe. Ila sababu za ujumla ni kuwa na kiwango kikubwa za kemikali tajwa katika mkojo, kupungua kwa wingi wa mkojo, kupata maambukizi katika mfumo wa mkojo (UTI) na kupungua kwa kemikali ambazo huzuia kutengenezeka kwa mawe.

1. Mawe ya calcium huzidi pale kiwango cha calcium kinapo kuwa kikubwa katika mkojo. Hii inaweza kutokana na kuongezeka kwa kiasi cha calcium inayochujwa na figo, au kuongezeka kwa calcium inayo ingia mwilini kutoka kwenye mfumo wa chakula

2. Mawe ya uric acid hutokea pia uric acid inapokuwa nyingi katika mkojo, hutokea kwa watu wenye magonjwa ya gout, watu wenye kisukari na watu wanene na wenye shida za insulin

3. Mawe ya struvite ni mawe yatokanayo na kuwa na maambukizi ya wadudu kwenye mfumo wa mkojo (UTI). Wadudu hawa huongeza pH ya mkojo ambayo ni hali rafiki kwa kutengeneza mawe

4. Mawe ya cysteine. Haya hutokana na shida katika vinasaba vya mtu vinavyo husika na uvunjwaji na usafirishaji wa kemikali ya cysteine

DALILI ZA MAWE KATIKA FIGO
Mawe kwenye mfumo wa mkojo huja kwa dalili tofauti ambazo hupelekea mtu kufika hospitali.

1. Maumivu makali sana ya tumbo maeneo ya pembeni chini ya mbavu ya ghafla
2. Kupata kichefu chefu na kutapika
3. Mkojo kuuma wakati wa kukojoa
4. Mkojo kuwa mchafu
5. Homa kama mtu ana UTI
6. Kutoka na damu kwenye mkojo
7. Baadhi ya mawe yanaweza yasiwe na dalili

VIPIMO
Utakapofika hospitali utafanyiwa vipimo tofauti kugundua aina ya jiwe ulilonalo, chanzo cha kuongezeka kwa kemikali husika.

MATIBABU
Asilimia kubwa ya mawe hutoka, ama hupita yenyewe kwenye mkojo mtu anapokojoa. Kwa wastani huchukua wiki moja hadi wiki tatu.
Hivyo basi sehemu kubwa ya matibabu ni kupunguza dalili tajwa na kusaidia kuweza pitisha jiwe. Matibabu haya ni kama; dawa za maumivu, dawa za kuongeza mkojo, dawa za kupandisha au kupunguza pH ya mokojo kulingana na aina ya jiwe. Mawe makubwa huzidi upana wa sentimita 1.5, yanaweza hitaji upasuaji kutolea.

Na sehemu ya pili ya matibabu ni katika kutibu chanzo mama cha kutengeneza jiwe. Chanzo sababishi cha kuzidi kwa kemikali katika mkojo ili kuzuia nafasi ya kujirudia kwa hali hii.
Inashauriwa mtu kujitahidi kunywa maji angalau lita 3 kwa siku ili kuongeza kiasi cha mkojo, kupunguza protini zitokanazo na vyakula kutoka kwa wanyama, kuwa na uzito mzuri, na kupata matibabu sahihi kwa wakati unapo kua na maambukizi au magonjwa tofauti.
Usidhani unapokua unavihatarishi vya kutengeneza mawe inamaananisha tayari unatatizo. Cha msingi zingatia kuepuka vihatarishi hivi.

1 thought on “Je ni kweli mawe kwenye figo husababishwa na kutokunywa maji tu?

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show