Zifahamu dalili za saratani ya ini.

 

Saratani ya ini ipo katika saratani kuu tatu ambazo zimekuwa zikisababisha vifo kwa wingi duniani. Maeneo ambayo yameathirika kwa wingi ni yale yaliyo na maambukizi makubwa ya vijidudu vinavyosababisha homa ya ini (Hepatitis “A”na “B”). Hivyo basi, kupata chanjo ya homa ya ini ni hatua kubwa katika kujikinga na ugonjwa huu.

Je, ni makundi yapi katika jamii ambayo yako katika hatari kubwa ya kupata maambukizi ya homa ya ini na hivyo basi kuweza kupelekea saratani ya ini hapo baadae?

 • wafanyakazi wa vituo vya huduma ya afya wanaofanya kazi katika mazingira karibu sana na damu na vimiminika vingine kutoka katika mwili wa binadamu.
 • kujamiiana na mpenzi mwenye wapenzi wengi.
 • watoto wachanga wanaozaliwa na mama mwenye maambukizi ya vijidudu vya homa ya ini
 • watu wanaojidunga sindano (mfano zile za madawa ya kulevya)

kuhusiana na dalili za saratani hii, kama zilivyo saratani nyingine, huwa katika hatua za mwanzoni mara nyingi huwa hazina dalili. Na hata baadae, dalili zake karibia zote hufanana na dalili za homa ya ini. Hivyo basi, vipimo husaidia kutofautisha kati ya hayo magonjwa mawili yenye uhusiano mkubwa.

 • Kuona uzito wako unapungua bila kuwa na sababu ya msingi
 • kupoteza hamu ya kula na kushiba haraka ukila chakula kidogo
 • kichefuchefu na kutapika
 • kuona tumbo lako linavimba kadri siku zinavyozidi kuendelea
 • kuwa na manjano kwenye weupe wa macho na baadae kuendelea hadi kwenye ngozi
 • maumivu ambayo sio makali katika sehemu ya juu-kulia mwa tumbo
 • Kutokwa na damu kwenye fizi pale unapopiga mswaki. Na mara nyingine kutokwa na damu pale unapopata michuboko midogo tu.

Dalili hizi haziko tu kwa ugonjwa wa saratani ya ini. Bali humtokea hata mtu wa magonjwa mengine hasa ya tumbo. Hivyo basi, ni vyema kwenda kwenye kituo cha afya mapema kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Jikinge, hakikisha wewe na familia yako mnapata chanjo ya homa ya ini”

 

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show