Inawezekana kumkinga mtoto wako na meno ya kahawia.


Siku zote kinga ni bora kuliko tiba na wazazi wengi wamekuwa wakitamani meno ya watoto wao ya kahawia yangeweza kuepukika.

Meno ya kahawia kitaalamu hujulikana kama dental florosis na meno haya husababishwa na kiwango kikubwa cha madini ya floridi kwenye maji au chakula katika kipindi ambacho meno ya mtoto yanatengenezwa.

Madini haya hupatikana kwenye maji ya kunywa au ya kupikia au kwenye vyakula kama mboga mboga zinazopandwa katika ardhi yenye madini haya.Nchini kwetu mikoa kama Arusha,Kilimanjaro,Singida,Shinyanga imeonekana kuwa na viwango vikubwa vya madini haya na watoto wengi huadhirika.

Kiwango salama cha madini ya floridi kwa binadamu kwenye chakula na maji ni 0.05 mpaka 0.07mg/F/kg/kwa siku.Kiasi chochote juu ya kiwango hiki husababisha kuongezeka kwa uwezekano wa kuwa na meno yaliyoathirika.

Kipindi ambacho meno hutengenezwa ni kati ya mwaka 1 mpaka miaka 4 ya mtoto na ndio kipindi hatarishi ambacho kinaweza kupelekea meno ya kahawia.

Mtoto anapofikia umri wa miaka 8 na kuendelea tayari anakuwa ametoka katika kipindi cha hatari ya kupata meno haya hata akiendelea kula au kunywa maji yenye kiwango kikubwa cha floridi.

Jinsi gani sasa unaweza kuzuia meno haya

  • Mama wajawazito na watoto walio na umri chini ya miaka minne waepuke kutumia maji au chakula chenye kiwango kikubwa cha madini ya floridi.
  • Watoto walioko chini ya miaka 5 wasimamiwe wakati wa kupiga mswaki kwa kutumia dawa ya meno yenye madini ya floridi.
  •  Pia kuepuka kutumia dawa ya meno yenye madini ya floridi kwa watoto walio na umri chini ya miaka 2 hadi pale daktari wa meno atakaposhauri.
  • Kwa watoto walio chini ya miaka 2 na wanahitaji kutiumia dawa ya meno,kiasi kidogo kama punje ya harage ndio itumike.
  • Usimamizi wa watoto walio chini ya miaka 6 ili wasimeze dawa ya meo wakati wakipiga mswaki.
  • Kitu ambacho serikali inaweza kufanya ni kupunguza kiwango cha madini ya floridi kwenye maji ya kunywa(de-fluoridation) kwenye maeneo ambayo madini haya yako kwa wingi(endemic areas) .

Ili kuepusha watoto wetu kuwa na hali hii ya meno ni jukumu letu kuwa mama wajawazito na watoto walioko chini ya miaka 6 wanapata maji ya kunywa na vyakula vyenye viwango vidogo vya floridi.

2 thoughts on “Inawezekana kumkinga mtoto wako na meno ya kahawia.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show