Kwanini napata maumivu wakati wa kufanya mapenzi!?

Maumivu wakati wa kufanya mapenzi yanaweza kuelezewa kama maumivu ayapatayo mwanamke kwenye sehemu za siri. Yanaweza kuwa ya muendelezo (persistent) au ya kujirudia (recurrent) aidha kabla, wakati au baada ya kufanya mapenzi. Wanawake wengi hupata tatizo hili walau wakati mmoja kwenye maisha yao.

Maumivu haya yaweza kuwa;

-Wakati tu uume unaingia
-Unapoingiza kitu chochote hata kidole
-Wakati uume ukiwa ndani
-Maumivu ya kupwita (throbbing pain) yanayodumu masaa kadhaa baada ya tendo.

Sababu za maumivu

Sababu zaweza kuwa za kimwili(physical) au za kisaikolojia.
Sababu za kimwili baadhi ni kama;

 • Kutokua na ute wa kutosha kwa ajili ya kulainisha uke kutokana na kukosa maandalizi ya kutosha, kupungua kwa homoni baada ya ukomo wa hedhi, kujifungua au kunyonyesha, baadhi ya dawa za magonjwa ya akili, presha na uzazi wa mpango.
 • Ajali au upasuaji maeneo ya nyonga, ukeketaji na kuongezewa njia wakati wa kujifungua. Pia matibabu ya kutumia mionzi eneo la nyonga.
 • Tatizo la mishipa ya uke kusinyaa yenyewe (Vaginismus).
 • Tatizo la uumbaji linalopelekea mtu kuzaliwa wakati uke haujatengenezwa vizuri mfano “vaginal agenesis na imperforate hymen.”
 • Magonjwa ya kizazi kama “endometriosis, PID,fibroids.”

Sababu za kisaikolojia baadhi ni kama; msongo wa mawazo, wasiwasi, sonona, matatizo ya mahusiano, woga wa mimba, historia ya kuumizwa kimapenzi (sexual abuse) siku za nyuma.

“Endapo una tatizo hili msaada unapatikana katika vituo vya afya na matibabu hutegemea na nini hasa kimepelekea wewe kupata tatizo hilo. Matibabu hayo yanaweza kuwa ni dawa au ushauri wa wewe na mwenza wako kushirikiana vizuri katika tendo hili.

4 thoughts on “Kwanini napata maumivu wakati wa kufanya mapenzi!?

 1. doctor, sijaelewa Kwenye sababu za maumivu wakati wa kujamiana kipengele cha “”uumbaji….more clarification plz…

  1. Asante Annie
   Sababu za uumbaji nimetoa mifano miwili ya vaginal agenesis na imperforate hymen.
   Vaginal agenesis ni kwamba uke unakua haujatengenezwa katika hatua za mwanzo za mabadiliko ya ukuaji wa mtoto akiwa tumboni. Kwahiyo unapojaribu kuingiza uume kwenye hali kama hii ambayo tundu la uke halipo matokeo ni maumivu tu.
   Imperforate hymen ni hali ya kwamba ule utando (membrane) unaoitwa hymen ambao kikawaida huwa na tundu katikati unakua umekosa tundu hilo na hivo mtu anavojaribu kuingiza uume mara akutanapo na ukinzani wa utando huo husababisha maumivu makali.
   Natumaini nimejibu vizuri; karibu sana Daktari Mkononi

  1. Asante sana Fortunata kwa swali zuri
   Katika sababu moja ya maumivu nimeeleza kuhusu kukosa maandalizi ya kutosha. Endapo utatumika muda wa kutosha kumuandaa mwanamke mpaka ute ule unaolainisha ukatengenezwa wa kutosha; ukubwa wa uume hautajalisha kabisa kwa sababu uke huwa unatanuka katika hali ya kawaida.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show