Sababu 5 zakuchelewa au kukosa hedhi

Unahofu kwa sababu umechelewa kuona siku zako, na unajua wewe si mjamzito? Kuchelewa kuona siku zako au kuzikosa hutokea kwa sababu nyingi ukiacha mimba.

Wanawake wengi huona siku zao baada ya siku 28. Ingawa mzunguko wa hedhi kwa kawaida huweza kutumia siku 21 hadi siku 35. Ikiwa hujapata hedhi katika kipindi hiki, zifuatazo huweza kuwa sababu:

1. Msongo wa mawazo
Msongo wa mawazo huweza kubadili homoni zako, kubadilisha ratiba yako ya kila siku, na hata kuathiri sehemu ya ubongo wako unaohusika na kumudu hedhi zako. Msongo wa mawazo huweza kusababisha ukaugua au uzito kushuka au kupanda, ambayo zote yanaweza kuathiri mzunguko wako wa hedhi.
Ikiwa unadhani una msongo wa mawazo jaribu kupumzika mara kwa mara, jaribu kufanya mazoezi pia.

2. Uzito mdogo au uliokithiri.
kuwa na uzito asilimia 10 chini ya uzito unaosemekana kuwa wa kawaida kwa urefu wako unaweza kubadilisha njia ya kawaida ya kupata hedhi.
Kama uzito mdogo wa mwili unaweza kusababisha mabadiliko ya homoni, hivyo hivyo pia inaweza kusababishwa na uzito mkubwa. kuwa na uzito wa kawaida hurudisha hedhi katika hali ya kawaida. kujua kama uzito wako ni sahihi ingia hapa:

http://daktarimkononi.com/2018/03/15/je-uzito-wako-ni-salama-kwa-afya-yako/

3. Vidonge vya uzazi wa mpango.
Unaweza kupata mabadiliko katika mzunguko wako wakati unatumia vidonge vya uzazi wa mpango. Vidonge hivi huwa na homoni ya estrogen na progesini, ambayo huzuia mayai yako kutoka. Inaweza kuchukua hadi miezi sita kwa mzunguko wako kurudi katika hali ya kawaida tena baada ya kuacha vidonge hivyo.

4. Magonjwa ya muda mrefu (ya kudumu)
Magonjwa ya muda mrefu kama kisukari yanaweza kuathiri mzunguko wako wa hedhi. Mabadiliko katika sukari katika damu yanauhusiano mkubwa na mabadiliko ya homoni, hivyo kisukari kisichodhibitiwa kinaweza kusababisha hedhi yako kubadilika.

5. Magonjwa ya Tezi ya thyroid

Tezi kutokufanya kazi au kufanya kazi sana huathiri mzunguko wa hedhi kwa kiasi kikubwa. Matatizo ya tezi hii huweza kutibiwa kwa dawa na hedhi ikarudi kama kawaida.

Tembelea link hii kufahamu ni dalili zipi zisizo salama na kukulazimu umuone daktari

HEDHI: Viashiria sita (6) vya kumuona Daktari

3 thoughts on “Sababu 5 zakuchelewa au kukosa hedhi

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show