Tatizo la Kushindwa Kusimamisha Uume

Uume kutosimama ni tatizo linaloweza kuwa ni kutofanikiwa kabisa kusimamisha au kushindwa kustahimili hali hiyo kwa muda wa kutosha unapofanya mapenzi. Wanaume wengi huathiriwa na tatizo hilo mara kadhaa kwenye maisha yao. Karibu 50% ya wanaume wenye umri zaidi ya miaka 40 hupata tatizo hili; hivyo huathiri ubora wa maisha yao.

Mwanaume mpaka apate msisimko wa mapenzi ; ubongo, vichochezi (hormones), hisia, mishipa ya fahamu, misuli na mishipa ya damu vinatakiwa kuhusika. Hitilafu katika moja ya sehemu hizo hupelekea kuwa chanzo cha tatizo hili, hitilafu zaweza kuwa za kimwili (physical) au za kisaikolojia.

Sababu za kimwili zaweza kuwa; magonjwa ya moyo, kisukari, mgandamizo mkubwa wa damu, kuwa na uzito mkubwa (obesity), pombe, sigara, madawa ya kulevya na baadhi ya madawa ya hospitali, matibabu ya tezi dume na upasuaji au ajali zinazoathiri maeneo ya nyonga au uti wa mgongo.

Sababu za kisaikolojia zaweza kuwa; wasiwasi kuhusu kazi, pesa, mahusiano yako, familia au hata wasiwasi wako kwamba unaweza usisimamishe uume, sonona (depression), msongo wa mawazo na matatizo mengine ya akili.

Madhara ya tatizo hili

-Kuwa na tatizo hili inaweza kupelekea kushindwa kumridhisha mwenza wako katika suala la mapenzi.
-Kupata msongo wa mawazo na wasiwasi zaidi.
-Kufedheheka na kushindwa kujiamini.
-Huweza kuleta matatizo na mvurugano katika mahusiano.
– Kushindwa kumpa mimba mwenza wako.

Njia za kuepuka tatizo hili

Kujiepusha na tatizo hili ni kufanyia kazi visababishi vyake, kwa mfano;

 • Hakikisha unadhibiti tatizo la kisukari na magonjwa ya moyo kama unayo.
 • Tembelea vituo vya afya mara kwa mara ili kufanyiwa uchunguzi.
 • Acha matumizi ya sigara na madawa ya kulevya, punguza matumizi ya pombe.
 • Chukua hatua kupunguza msongo wa mawazo.
 • Fanya mazoezi mara kwa mara na pata lishe bora kujiepusha na uzito mkubwa.

“Upatapo tatizo hili usione aibu wala kujificha bali fika katika kituo cha afya ambapo daktari atachukua maelezo yako na kukupa msaada wa kitaalamu kulingana na sababu iliyoopelekea mpaka ukapata tatizo hili.

6 thoughts on “Tatizo la Kushindwa Kusimamisha Uume

 1. Asante sana dokta kwa maelezo mazuri,eti ni kweli kama mpenzi wako hakuvutii unaweza kushindwa kusimamisha uume?!

  Na je kuna uhusiano wowote kati ya uchovu wa kutokana na kazi na tatizo hili?yaani mfano mtu anatoka kazini amechoka bas akifika nyumbani anakuwa hawezi kusimamisha na kushiriki tendo.

  1. Asante sana Millaine
   Kama umesoma makala kwa umakini nimeelezea kwamba kuanzia ubongo, mishipa ya fahamu, hisia, mishipa ya damu na misuli vyote vinatakiwa kwenda sawa ndipo uume usimame.
   Inapotokea basi hali kama hiyo kwamba mtu hakuvutii basi hapo suala la hisia linachukua nafasi, vilevile uchovu baada ya kazi hupelekea ubongo pia kuchoka na hivyo nafasi yake katika kuleta ufanisi wa uume kusimama inapungua.
   Natumaini nimekujibu vyema; karibu sana Daktari Mkononi

 2. Asante Dr kwa somo zuri.
  Tezi dume imekuwa ni gumzo kubwa hasa kwa watu wenye umri mkubwa…na matibabu yake kama ulivo indicate ni moja kati ya sababu ya kushindwa kusimamisha uume..
  Je kuna matibabu ya aina yoyote ambayo mtu mwenye tezi dume anaweza kupata bila kuathiri uwezo wake wa kusimamisha uume?
  Asante

  1. Asante sana Job kwa swali lako lililojieleza vizuri;
   Watu wengi wanaopatwa na tatizo la tezi dume kwanza huwa na umri mkubwa kama ulivosema na hivyo baada ya upasuaji huo sababu za uume kutosimama zinaweza kuwa ni kuharibu mishipa ya fahamu au umri wenyewe. Njia mbalimbali kama upasuaji kwa kupitia tumboni, kutumia mionzi vimejaribiwa lakini matokeo yake yanamtegemea na uangalizi wa karibu wa mgonjwa baada ya procedure hiyo.
   Study imefanyika katika chuo cha Johns Hopkins na kimebaini haya, kwa kujifunza zaidi unaweza kutembelea link ifiatayo
   https://www.google.com/url?sa=t&source=web&rct=j&url=http://urology.jhu.edu/erectileDysfunction/erectile_dysfunctions_RP.php&ved=0ahUKEwiHuIiqrPXZAhXTasAKHUPxDUgQFghDMAE&usg=AOvVaw3y1a3cSi1_DWhdmnwA8RRQ

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show