Ifahamu Homa ya Dengue

Ugonjwa huu wa homa ya dengue uliwahi kujitokeza mwaka 2014 ambapo zaidi ya watu 400 katika mji wa Dar es Salaam waligundulika kuwa na homa ya dengue na 3 waliripotiwa kufariki.

Fahamu kuhusu Ugonjwa wa Homa ya Dengue

Homa ya dengue ni ugonjwa unaosababishwa na virusi na unaosambazwa na mbu. Kwa watu wengi, ugonjwa huu hauna madhara makubwa na huchukua takribani wiki 1 kabla ya kupona wenyewe. Lakini kwa baadhi, huweza kuwa kali na kuhatarisha maisha ya muathirika.

Dalili za Homa ya Dengue

Dalili huanza ghafla siku 4 hadi 10 tangu kuambukizwa. Dalili hizi ni kama:

 • Homa kali, joto la mwili hufika hadi 40C na zaidi
 • Kichwa kuuma sana
 • Maumivu ya viungo, misuli na nyuma ya macho
 • Hali ya uchovu
 • Mwasho mwilini na rangi ya ngozi kuwa nyekundu
 • Kukosa hamu ya kula

Dalili hizi huchukua takribani wiki 1 ingawa hali ya kujisikia kuumwa huweza kuendelea wiki kadhaa baadae.

Dalili za hatari za homa ya dengue

Kwa baadhi ya watu, ugonjwa huu unaweza kuwa mkali kuliko kawaida, hasa kama unajirudia. Dalili za kuashiria homa kali ya dengue ni:

 • Tumbo kuwa kubwa na kuuma sana
 • Kutapika mara kwa mara / Kutapika damu
 • Kutokwa na damu kwenye fizi za meno au chini ya ngozi
 • Kupata shida kupumua
 • Ngozi kuwa ya baridi
 • Kuhisi mapigo ya moyo kupungua
 • Uchovu usio wa kawaida au kupoteza fahamu

Pindi unapoona dalili hizi, wahi hospitali kwa matibabu zaidi.

Unaambukizwaje?

Homa ya dengue huambukizwa kwa kung’atwa na mbu aina ya “Aedes” wenye virusi  hivi. Mbu hawa hung’ata muda wowote wakati wa mchana, hasa mapema asubuhi au jioni kabla jua kuzama, tofauti na mbu wanaoeneza malaria ambao hung’ata wakati wa usiku. Mbu hawa hupatikana maeneo yenye maji tulivu kama kisimani, kwenye mapipa nk.

Image processed by CodeCarvings Piczard ### FREE Community Edition ### on 2017-10-30 14:43:33Z | http://piczard.com | http://codecarvings.com

Aina mbalimbali za mbu “Aedes” wanaoeneza ugonjwa wa homa ya dengue

Homa ya dengue haienezwi kutoka mtu mmoja hadi mwingine. Pia waweza kuupata ugonjwa huu tena, hata kama umewahi kuumwa kabla.

Tiba ya Homa ya Dengue

Hakuna dawa au tiba ya homa ya dengue. Njia pekee ni kudhibiti dalili zake pindi zinapoanza kujitokeza. Waweza kufanya yafuatayo:

 • Tumia dawa za kutuliza maumivu na homa mfano Paracetamol. Usitumie dawa za aspirin au ibuprofen kwa kuwa huchochea kutokwa na damu zaidi.
 • Kunywa maji mengi
 • Pumzika vya kutosha

Jinsi ya kujikinga na homa ya dengue

Njia bora zaidi ni kujiepusha kung’atwa na mbu. Waweza kufanya yafuatayo:

 • Tumia dawa za kufukuza mbu (insect repellent)
 • Vaa nguo zisizobana. Mbu hawa huweza kufikia ngozi kama nguo zimeshikamana sana na mwili. Pia vaa nguo zinazofunika sehemu za mwili kama mikono na miguu mfano suruali, mashati yenye mikono mirefu, soksi na viatu vinavyofunika miguu
 • Lala ndani ya chandarua iliyotiwa dawa
 • Hakikisha mazingira ya nyumbani yapo salama kwa kufyeka majani marefu na kuondoa vyanzo vya maji tulivu

 

1 thought on “Ifahamu Homa ya Dengue

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show