MSOKOTO KWA WATOTO WACHANGA (BABY/INFANTILE COLIC)

Je,msokoto ni nini na huja kivipi?
Msokoto wa njia ya chakula ni jambo la kawaida kwa watoto wachanga.Takriban asilimia 10 hadi 40 ya watoto wachanga walio katika umri wa wiki mbili hadi miezi sita hupatwa na msokoto.Jambo hili husababisha watoto kulia kupita kiasi na kuwapa hofu wazazi.Kuna hatari ya mtoto kupewa tiba zisizohitajika ama zisizofaa.

Kiini haswa kisababishacho msokoto hakijulikani ingawa madaktari wanakisia kuwa ni juu ya mabadiliko katika njia ya chakula mtoto mchanga anapokua.Mabadiliko haya yanaweza kufanya utumbo wa mtoto kujikaza na kulegea kwa ghafla(hyperperistalsis) jambo ambalo huleta uchungu na kulia kwingi

Kwa kawaida mtoto mchanga aliyeshiba na asiye mgonjwa anafaa kulia kwa ujumla wa masaa mawili kwa siku.Watoto wakiwa na msokoto hulia kupita kiasi hususan nyakati za jioni.Kilio hiki hua cha sauti ya juu ipenyezayo masikioni.Mara nyingi juhudi za kumtuliza mtoto hua hazionekani kuleta afueni yoyote.
Dalili na ishara za msokoto.
Wataalamu wa afya wameelezea kuwa ili mtu ujue kama kulia kupita kiasi kunatokana na msokoto,lazima kutimize vipengele vifuatavyo:
Mtoto kulia zaidi ya masaa matatu kwa siku kiujumla.Sanasana nyakati za jioni.
Kulia ni zaidi ya siku tatu kwa wiki.
Kulia huku kumekua kwa wiki tatu ama zaidi.
Mtoto hana ugonjwa wowote-mambo yanayohashiria ugonjwa ni kama;wingi wa joto mwilini,mtoto kuwa mdhoofu na kunyonya kwaunyonge,kutapika,kuendesha ama kufura tumbo na mtoto kupoteza uzani.
Mtoto hasiwe na njaa.

Mambo mengine ambayo huambatana na kulia ni kama:
Mtoto kuinua miguu hadi tumboni.
Mtoto kukunja ngumi.
Mtoto kupiga matuta kwenye kipaji.
Wekundu wa ngozi usoni(flushing).

Mzazi anapaswa kufanya nini akigundua mtoto wake mchanga ana msokoto?
Msokoto hauna madhara yoyote ya muda mrefu kwa mtoto na hujiponya wenyewe(it`s self-limiting) kabla mtoto afikishe umri wa mwaka mmoja.

Kwa wakati huu,hakuna dawa yoyote inayotambulika kuponya msokoto.Wazazi wanashauriwa kutompa mtoto dawa yoyote iwepo ya kienyeji ama ya kisasa kwani zinaweza kumdhuru kiafya.

Mzazi anaezafanya mambo yafuatayo kujaribu kumtuliza mtoto akiwa na msokoto:
Kumshika mtoto kwa upande chini ya mbavu ama mgongoni.
Kubembeleza mtoto huku ukimtolea sauti za kumuongoa.
Kunyonyesha mtoto.
Si jambo la busara kujaribu kumkanda mtoto tumboni anapokua na msokoto.

Mama anayenyonyesha mtoto huyo anafaa kuacha kutumia maziwa,mayai na njugu.Jambo hili limenguduliwa kupunguza ukali wa msokoto mtotoni.

Mtoto pia hafai kuwa katika mazingira yaliyo na moshi wa sigara kwani  inamueka katika hali ya kupata msokoto kwa urahisi.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show