Jinsi earphones zinavyoharibu masikio yako

 

Katika zama za sasa hivi na ukuaji wa teknolojia, uvaaji wa earphones umeongezeka na unazidi kuongezeka kwa kasi kubwa. Uvaaji wa earphones sio mbaya, lakini asilimia kubwa ya watu hutumia earphones kwa makosa na kuweka masikio yao katika hatari kubwa hasa kwa miaka kadhaa ijayo.

Athari kuu za utumiaji wa earphones ni pamoja na :

 • Kushindwa kusikia. Pale unapotumia earphones na kusikiliza muziki katika sauti ya juu, unakua unaua ule uwezo wa kusikia ambao ulikuwa umezaliwa nao. Kujua kuwa sauti iko juu, kuna baadhi ya simu huokuonesha kuwa sauti iko juu sana. Na unaweza kugundua pia pale unapovaa earphones na mtu aliye jirani yako kama na yeye anauwezo wa kusikia yale unayoyasikiliza.
 • Magonjwa ya masikio. Magonjwa haya ni hasa ya sehemu ya nje ya sikio. Hili hutokea sana kwa njia ya kushirikiana earphones na mtu mwingine. Hii hutoa maambukizi kutoka kwake na kuleta kwako.
 • Kuziba hewa isiingie ndani ya masikio. Hivyo basi kupelekea uchafu kushindwa kutoka kama ilivyo kawaida. Hivyo kueka hatari ya sikio kuziba
 • kutosikia kwa mda. Hii hutokea mara tu baada ya kusikiliza sauti ya juu kwa mda mrefu. Lakini hali hii hutoweka mara baada ya mda mchache. Kujirudirudia kwa hali hii hupelekea kushindwa kusikia kabisa hapo baadae.
 • Sikio kuuma. Hii hasa baada ya kusikia sauti ya juu. Mda mwingine hupelekea kusika sauti za “zzzzzz”
 • Hatari ya ajali. Uvaaji wa earphones ukiwa unatembea barabarani huzuia usisikie yale yanayoendelea na hivyo huweza pelekea ajali hasa wakati wa kuvuka barabara.

Hivyo basi, tumia earphones zako ki-Afya zaidi kwa:

 • Kusikiliza kwa sauti usiyo ja juu
 • Kutoshirikiana earphones zako na mtu mwingine
 • Usivae earphones kwa mda mrefu
 • Usivae earphones ukiwa unavuka barabara au kuendesha gari .

Yatunze masikio yako. “Nenda kafanyiwe uchunguzi wa masikio yako kwa mtaalamu wa masiko angalau mara moja kila mwaka”

 

2 thoughts on “Jinsi earphones zinavyoharibu masikio yako

 1. Asante sana Daktari, umeelezea vizuri kwa kweli na nimeelewa. Natumaini leo kwa ujumbe huu utakua umeokoa masikio ya watanzania wengi
  Kazi nzuri

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show