Matumizi mabaya ya dawa za usingizi (Valium)

Valium ni moja kati ya dawa maarufu sana ambayo hutumiwa na watu wengi kwa ajili ya kutibu tatizo la kukosa usingizi.

Dawa hizi zikitumiwa kwa kipindi kirefu humfanya mtumiaji kupata utegemezi wa dawa hizi ambao ni hatari kwa afya ya mtumiaji.

Utegemezi huu (dependency) hutegemeana na mfumo wa maisha ya mtumiaji wa dawa hizi, kwa mfano mtu atumiae Pombe (Mlevi) na dawa hizi (valium) kwa pamoja yuko kwenye hatari ya kupata utegemezi wa dawa hizi tofauti na mtu asiyetumia pombe ambaye uwezekano wa kupata utegemezi wa dawa hizi ni mdogo.

Je ni nini madhara kama mtegemezi wa dawa hizi ataacha kuzitumia dawa hizi kwa mara moja? (withdraw effects).

1.Viungo kukakamaa na kushindwa kufanya kazi ama kutembea.
2. Kukosa usingizi kabisa.
3. Kuchanganyikiwa.
4. Maumivu makali ya kichwa na viungo vyote vya mwili.
5. Kichefuchefu na kutapika.
6. Kizunguzungu na kupata kichaa.

  • Hakikisha kabla ya kuanza kutumia dawa hizi unapata ushauri kutoka kwa muhudumu wa kituo cha afya na pia mara baada ya kumaliza dozi ya dawa hizi toa taarifa kwa mhudumu wa kituo cha afya kwa ajili ya ushauri zaidi.

Kumbuka dawa hutibu magonjwa lakini pia ni sumu kama zisipotumika ipasavyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show