Uhusiano kati ya ugonjwa wa moyo wa infective endocarditis na matibabu ya meno

Infective endocarditis(I.E) ni ugonjwa wa moyo  unaohatarisha maisha wenye  uhisiano mkubwa na matibabu ya  kinywa na meno kwa watu wenye magonjwa ya moyo.Soma hapa http://daktarimkononi.com kujua zaidi kuhusu ugonjwa huu.

Tafiti za kisayansi zimeonesha kuwa IE   una hatarisha maisha kwa zaidi  ya asilimia 30.Ugonjwa huu hutokea pale bakteria wanaopatikana kinywani na kawaida huwa hawana madhara katika kinywa(normal flora) au bakteria wengine waliosababisha maambukizi kinywani wanapoingia kwenye mishipa ya damu na kufika kwenye moyo hivyo kusababisha madhara kwenye kuta za valvu za moyo kuziharibu kabisa.

Kitendo cha bakteria hawa kutoka mdomoni na kuingia kwenye mfumo wa damu kinaweza kutokea wakati wa kufanyiwa baadhi ya matibabu ya kinywa na meno mfano kusafisha ugaga kwenye meno(scalling and root planing),kung’oa jino,kuziba jino mpaka kwenye mzizi(root canal) au hata kuingiziwa vifaa vya uchunguzi kwenye fizi(probing).Pia inaweza kutokea pale mgonjwa anapopiga mswaki na kutoka damu kwenye fizi,kuwa jino lilitoboka mpaka kwenye mzizi(deep dentinal caries with pulp involvement) hii inaweza kuwapa bakteria hawa njia ya kuingia kwenye damu.

Watu  wafuatayo wapo kwenye hatari ya kupata ugonjwa huu kutoka kwenye fizi zao au kinywa kizima.

  • Watoto waliozaliwa na magonjwa ya moyo(congenital heart diseases)
  • Mtu ambaye ana historia ya ugonjwa wowote wa moyo
  • Mtu mwenye kipandikizi kwenye moyo(implants) au aliyepandikiziwa moyo(heart transplant)
  • Mtu ambaye amefanyiwa upasuaji wowote wa moyo siku za karibuni hasa ndani ya miezi 6.
  • Mtu mwenye valvu za moyo za kupandikiziwa(prosthetic valves)

Wagonjwa wa moyo wanashauriwa kutunza vyema afya ya kinywa na meno yao kwani wapo kwenye hatari ya kupata ugonjwa huu.Hivo wanashauriwa kufanya yafuatayo…

  • Kupiga mswaki vizuri angalau mara 2 kwa siku.
  • Kutumia kamba za kusafishia meno(dental floss) angalau mara moja kwa siku
  • Kufanyiwa uchunguzi wa mara kwa mara wa kinywa na meno ili kutibu magonjwa ya kinywa mapema.
  • Kuhudhuria kliniki yako ya  moyo mara kwa mara ili kujua maendeleo yako.

Inashauriwa kila mgonjwa wa moyo kutoa taarifa mapema kuwa yeye ni mgonjwa kila anapokwenda kwa daktari wa meno ili kupatiwa  dawa za kujikinga na ugonjwa huu(antibiotic prophylaxis) saa moja kabla ya kufanyiwa matibabu au vipimo vyovyote vinavyohusisha kuingiza vifaa ndani ya fizi au vitakavyosababisha damu kutoka.

Unapokwenda kumuona daktari wa meno wasiliana kwanza na daktari wako wa moyo ili akupe ushauri kulingana na hali yako kwa wakati ule,ni vizuri pia kama daktari wako wa meno akawasiliana na daktari wako wa moyo kujiridhisha na

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show