Madhara ya afya yatokanayo na nyama choma.

Kuchoma nyama au kuipika kwenye moto mkali husababisha kutengenezwa kwa kemikali zinazo sababisha kansa. Kemikali hizi hutokana na virutubisho vya aina ya protini vilivyopo kwenye nyama vinapo kutana na moto mkali, pia moshi unaotokana na kuchoma nyama na vipande vidogo vidogo vyeusi vinavyo ganda kenye nyama. Kemikali hizi husababisha mabadiliko kwenye vinasaba vya mwili na kuleta kansa.

Inaongeza hatari ya kupata kansa za sehemu za mwili zifuatazo;
1. Kongosho
2. Tumbo
3. Matiti
4. Utumbo mkubwa wa chakula
5. Tezi dume

Nini tufanye kupunguza madhara yatokanayo na nyama choma

1. Epuka kupika/ kuchoma nyama kwa muda mrefu haswa kwenye moto mkali. Jinsi inavyokaa kwenye moto kwa muda mrefu ndivyo inavyozidi kutengeneza kemikali hatari.

2. Ongeza umbali/nafasi kati ya nyama na na jiko la kuchomea ili moto usiguse moja kwa moja kwenye nyama.

3. Weka nyama kwenye microwave angalau dakika 2 kisha unaichoma. Hii itapunguza muda wa kuchoma hivyo kupunguza kutengeneza kemikali hatarishi.

4. Weka mchanganyiko wa viungo kwenye nyama angalau kwa dakika 30 kisha ichome. Utafiti unaonesha kuwa viungo vinapunguza kutengeneza kemikali hatarishi.

5. Weka nyama kwenye foili, itoboetoboe kisha choma. Hii inasaidia kwasababu nyama haita kutana na moto moja kwa moja.

6. Wakati wa kuchoma weka vipande vidogovidogo ili iive haraka, wakatai wa kula hakikisha umeondoa ule weusi ulioganda kwenye nyama.

7. Safisha jiko lako la kuchomea nyama vizuri kabla ya kuchoma nyama mara nyingine tena, ili mabaki ya uchafu yasi gandamane na nyama yako na kuifanya kua nyeusi.

“Jambo zuri zaidi ni kuacha au kupunguza kiasi cha kula nyama choma. Pia waweza choma mboga za majani au matunda kupata ladha ya nyama choma, kwasababu hizi hazitengenezi kemikali hatarishi kama zile za kwenye nyama. Kama ni vigumu kuacha basi mchoma nyama inabidi awe na elimu ya hapo juu au zaidi jinsi ya kuchoma nyama vizuri, ikawa tamu bila kuhatarisha afya yako.”

9 thoughts on “Madhara ya afya yatokanayo na nyama choma.

  1. Asante Trae kwa swali zuri. Maelezo hayo ni kutokana na tafiti zilizofanywa na wana sayansi wanao husika na lishe na pia na kitengo cha kansa kutoka nchi mbalimbali.

   Na si kwamba ukila siku moja au mbili unapata kansa. Kansa ni ugonjwa unaochukua muda mrefu kujionesha hivyo kula kwa wingi na kwa muda mrefu ndio inaweza kusababisha kansa.
   Na nyama choma sio sababu pekee ya kansa, ila ni moja wapo ya vyakula ambavyo si vizuri kiafya.
   Nimatumaini yangu nimejibu swali vizuri…labda uwe more specific as in what kind of evidence do you want eg studies, research, link ya articles mbalimbali .?
   Karibu sana daktari mkononi.

 1. Asante daktari umetuelimisha vizuri ingawa jambo hili siyo rahisi sana kutekeleza. Tutajitahidi kwa kweli

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show