Faida za kunywa chai ya tangawizi

Je, unafahamu ni vitu vingapi unavipata unapokunywa chai ya tangawizi? Mbali na harufu nzuri na ladha pekee ni baadhi tu, vifuatavyo ni vitu unavyofaidika ukinywa chai

1: Hupunguza kutapika na kujisikia vibaya wakati wa safari.
Ukinywa chai yenye tangawizi inapunguza kutapika wakati wa safari kwa asilimia kubwa, hata unapoanza kujisikia vibaya, kunywa chai ya tangawizi, itapunguza kujisikia vibaya wakati wa kusafiri.
2: Husaidia kupunguza maumivu wakati wa hedhi
Kwa mtu anayepata maumivu wakati hedhi, chemsha maji ya tangawizi, loweka taulo na uliweke juu ya tumbo. Pia kunywa chai ya tangawizi iliyowekewa asali. Hii husaidia misuli ya tumbo kutokaza na huleta afadhali.
3: Hupunguza msongo wa mawazo.
Tangawizi husaidia kumtuliza mtu na kupunguza msongo wa mawazo.
4:Husaidia katika mmeng’enyo wa chakula.
Husaidia mmeng’enyo na kuongeza kasi ya chakula kufyonzwa mwilini. Pia husaidia kupata uafadhali baada ya kuvimbiwa.
5:Hupunguza yabisi (uvimbe)
Tangawizi hupunguza maumivu ya viungo na misuli kama ikitumika mara kwa mara. Unaweza ukaitumia kuiloweka na kuchua sehemu husika na ikapunguza yabisi
6: Hupunguza shida za mfumo wa upumuaji.
Chai ya tangawizi huleta afadhali kwa mtu mwenye dalili za mafua au kikohozi. Kama endapo mafua yametokana na mabadiliko ya kimazingira chai ya tangawizi hutoa msaada mkubwa.
7: Huimarisha kinga ya mwili, kwani inabaadhi ya madini ambayo huimarisha kinga


Faith Custor MD3 πŸ‡ΉπŸ‡Ώ

Work smart not hard 😎😎

All author posts

Privacy Preference Center