Vijue vyakula vinavyofaa baada ya mazoezi

Wengi huwa tunafikiria zaidi tule nini kabla ya kufanya mazoezi na sio baada ya mazoezi. Ila katika uhalisia kile unachokula kabla,wakati wa mazoezi na baada ya mazoezi vyote hujumuika kuleta matokeo mazuri zaidi .

Kwa kawaida unapokuwa unafanya mazoezi misuli yako hutumia sukari iliyopo kwenye misuli inaitwa glycogen na hivyo kuipunguza; vile vile protini zinazojenga misuli huvunjwa wakati wa mazoezi. Hivyo basi ni vyema kula vyakula vitakavyoongeza kiwango  cha sukari na kurudisha protini ya misuli yako.

Ulaji sahihi baada ya mazoezi huwa na faida zifuatazo;

-Hupunguza kiwango cha protini inayovunjwa katika misuli

-Hufanisisha ukuaji na kujengeka kwa misuli

-Hurudisha viwango vya glycogen

Vyakula hivi  vinavyofaa pia huwa ni vyakula vinavyoweza kumeng’enywa kwa urahisi na kutumika mwilini ndani ya muda mfupi.

Vyakula hivyo ni kama ;

a)matunda kama nanasi,parachichi,embe n.k

b)viazi hasa viazi vitamu

c)mbogamboga

d)mayai

e)maziwa angalau glasi moja

f)maji ya kutosha ,juisi ya chungwa au nanasi

g)maji ya madafu pia hufaa kwa kuwa yana kiwango kidogo cha sukari na huburudisha.

Inashauriwa, kula angalau dakika 45 baada ya mazoezi na ijulikane kuwa ni vyema kula vizuri hata baada ya mazoezi ili kupata malengo sahihi ya mazoezi yako.

4 thoughts on “Vijue vyakula vinavyofaa baada ya mazoezi

    1. Habari kaka Feisal,shukrani kwa kufuatilia makala zetu na asante kwa swali.inashauriwa ufanye mazoezi walau saa moja mpaka mawili baada ya kula ili kuruhusu muda wa kutosha kwa ajili ya chakula kumeng’enywa na tumbo kuwa wazi,ambapo hii pia itaepusha kutapika au kupata vichomi wakati wa zoezi na zaidi kukupa uhuru unapofanya mazoezi.
      Asante

  1. Asante kwa swali zuri ndugu Frank! Kwa kawaida, inashauriwa kula au kunywa muda usiopungua saa moja kabla ya mazoezi ambapo utahitajika kula vyakula ambavyo ni simple kama matunda. mfano mzuri ni ndizi ambazo zitakusaidia kuongeza madini chumvi kama sodium ambayo hutoka na jasho. Matunda haya unaweza tumia katika mfumo wakebwa kawaida au ukatengeneza juisi.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show