Fahamu juu ya njia ya uzazi wa mpango iitwayo kipandikizi.

Kuna njia nyingi za uzazi wa mpango zikiwemo kutumia vidonge, sindano, kondomu, kitanzi, kipandikizi na njia nyingine nyingi. Leo tuongelee kwa undani kuhusu kipandikizi.

Kipandikizi ni nini?

Kipandikizi ni njia ya uzazi wa mpango ambayo huwekwa kwenye sehemu ya juu ya mkono wa mwanamke usiotumika sana. Kipandikizi hufanya kazi kwa ufasaha kwa muda wa miaka mitatu hivyo kufanya iwe njia inayochaguliwa na wengi hasa wanaojisahau kunywa vidonge mara kwa mara.

Takwimu zinaonyesha kuwa Kipandikizi huzuia ujauzito kwa asilimia zaidi ya 99%

Faida za kipandikizi ni zipi?

•Hukaa na kufanya kazi kwa muda mrefu na uwezekano wa kupata ujauzito ni mdogo.

•Huna hofu ya kusahau kunywa dawa.

•Uwezo wa kushika ujauzito hurudi muda mfupi baada ya kutoa kipandikizi.

Madhara ya kutumia kipandikizi ni yapi?

•Maumivu wakati wa kukipandikiza.

•Kichwa kuuma.

•Kuongezeka uzito.

•Mabadiliko ya hisia.

•Maumivu ya tumbo.

•Kutokwa na damu ukeni usio wa kawaida.

Nani atumie kipandikizi?

•Wasichana.

•Wamama ambao hawajawahi kupata ujauzito na hata wenye watoto tayari.

•Wamama wanaonyonyesha.

Nani hashauriwi kutumia kipandikizi?

•Mama mjamzito.

•Mama mwenye ugonjwa wa ini.

•Mama mwenye historia ya kansa ya ziwa.

•Kutokwa na damu ukeni isivyo kawaida ambao bado haujajulikana chanzo chake.

•Kama una alleji na vipandikizi.

•Wamama wanaovuta sigara, wenye magonjwa ya moyo au kisukari.

TAHADHARI:

Kipandikizi hakizuii magonjwa ya zinaa hivyo kuna haja ya kutumia kinga iwapo mwanamke hana imani na mwenza wake.

4 thoughts on “Fahamu juu ya njia ya uzazi wa mpango iitwayo kipandikizi.

  1. Naomba kuuliza swali lililo nje kidogo ya topic.

    Njia ya majira ni salama kwa asilimia 100%? (Kama tarehe zitahesabiwa kwa ufasaha na kufanya tendo wakati wa tarehe salama). Je kuna uwezekano wa kupata mimba kama tendo litafanyika katika tarehe ambazo mwanamke yupo salama?

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show