Ifahamu mimba zabibu (sehemu A)

Pengine hii sio hali iliyozoeleka kusikika masikioni mwa wengi na pengine ni mara ya kwanza kusikia hali hii ya mimba zabibu, kitaalamu molar pregnancy. Hili ni tatizo katika kondo la uzazi(placenta) ambalo hujitokeza pale ambapo mbegu za kiume huungana na yai. Mimba zabibu ni uvimbe unaotokea katika mji wa uzazi na hukua kwa haraka zaidi ya mimba ya kawaida. Mimba hizi huleta dalili za mimba. Uvimbe wa mimba zabibu sio saratani lakini baadhi ya wanawake huwa katika hatari ya uvimbe huu kuwa saratani.
Chanzo cha mimba zabibu.
Kitaalamu mimba zabibu huwa za aina mbili,complete mole na partial mole.

•Complete mole ni mimba zabibu ambazo mbegu za kiume hurutubisha yai lisilo na vinasaba. Hivyo hupelekea mji wa uzazi kuwa na uvimbe usio wa kawaida tu bila mtoto kutengenezeka.

•Partial mole ni mimba zabibu ambazo mbegu za kiume hurutubisha yai lenye vinasaba, mwili wa mtoto kutengenezeka lakini pia mji wa uzazi unakuwa na tishu zabibu ambazo si za kawaida na hupelekea mtoto kufariki

Je, ni nani yuko hatarini kupata mimba zabibu?

Tafiti mbalimbali zimefanyika kujaribu kuidhinisha ni vitu gani huongeza hatari ya mama kupata mimba zabibu, hakuna chanzo kimoja kinachotajwa kuleta mimba zabibu bali ziko sababu mbalimbali ambazo huongeza hatari ya mama kuleta hali hii. Vitu hivi ni kama;
•Umri mkubwa wa mama, baadhi ya tafiti huonyesha umri mkubwa zaidi ya miaka 40

•Mama mwenye historia ya kupata mimba zabibu katika mimba zake zilizopita.

•Baadhi ya tafiti huonyesha upungufu wa virutubisho kama folic acid na vitamini A (carotene) kwa mama huongeza hatari ya kupata hali hii

•Tafiti zingine huonyesha vitu kama uvutaji sigara kuongeza hatari ya hali hii.

Si kila mwanamke mwenye sababu tajwa hapo juu kupata mimba zabibu, hivyo tafiti zaidi zinaendelea katika eneo hili.

Itaendelea..

Reviewed by Dr. Msiry

3 thoughts on “Ifahamu mimba zabibu (sehemu A)

  1. This knowledge is new for me, I would love to know more about it. Please do attach other useful sites so that we can understand the subject matter in full.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show