Kutokwa na damu nyingi kuzidi kiasi baada ya kujifungua.

Pengine sio mara ya kwanza kwa wengi wetu kusikia kuhusu hili tatizo,kwa kitaalamu linajulikana kama POST PARTUM HAEMORRHAGE(PPH).

Tatizo hili ni moja ya sababu kubwa sana ya vifo vya wakina mama vinavyotokea pindi na ndani ya masaa kadhaa baada ya mama kujifungua.

Tatizo hili limegawanyika katika sehemu mbili:

  1. Kutokwa na damu nyingi wakati wa kujifungua na ndani ya masaa 24 baada ya kujifungua (Primary PPH).
  2. Kutokwa na damu nyingi masaa 24 baada ya kujifungua(Secondary PPH)

Je ni kiwango gani cha damu huhesabiwa kama nyingi kuzidi kiasi?

Mwanamke akijifungua kwa njia ya kawaida akapoteza damu 500ml (nusu lita) au zaidi na 1000ml (lita moja) au zaidi iwapo atajifungua kwa operation.

Je nini husababisha mwanamke kutokwa na damu nyingi kuzidi kiasi?

  1. Mfuko wa uzazi kushindwa kusinyaa baada ya mtoto kutoka.
  2. Kushindwa kutoka/kubakia kwa vipande vya kondo la nyuma la uzazi (placenta) baada ya mtoto kutoka.
  3. Mtoto kuzuiwa kutoka katika kipindi cha kujifungua kupelekea kukaa muda mrefu katika njia ya uzazi (Prolonged 2nd stage of labour)
  4. Kujipandikiza vibaya kwa kondo la nyuma la uzazi(placenta accreta)
  5. Kuchanika au michubuko katika njia za uzazi (cervical/vaginal lacerations or tears)
  6. Utumiaji wa vifaa vya kusaidia mama kutoa motto (foceps/vacuum machine)
  7. Kuzaa mtoto mkubwa sana (Zaidi ya 4.5kgs)
  8. Kupasuka kwa mfuko wa uzazi (placenta tear).

Kutokana na uzito na ukubwa wa tatizo hili kina mama wajawazito wanashauriwa kujifungua katika kituo cha afya, ambapo wataalamu wa afya wanaweza kuzuia tatizo hili kutokea na pia kukabiliana nalo iwapo litajitokeza kwa kutoa matibabu stahiki kuokoa maisha ya mama na mtoto.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show