Ni mapema sana kwa mwanangu kuoza meno kiasi hiki!!.

  • Watu wengi hudhani kuwa watoto wakiwa na miezi michache tu, au katika kipindi cha kuonyonya maziwa ya mama pekee ni vigumu kwao kuoza meno. Lakini tafiti zinaonesha kuwa watoto chini ya miezi 71(chini ya miaka sita)  wanaweza kupata tatizo hili la kutoboka kwa meno, kutokuwa na meno sababu ya kungolewa baada ya kuoza au mengine kuzibwa. 
  • Kitaalamu tatizo hili huitwa Early Childhood Caries (ECC) au Rampant caries na mfano wake ndio huo hapo katika picha ya juu. 

Tafiti za kisayansi zilizofanywa zimeonesha kuwa 26.4% ya watoto kati ya umri wa miezi 6 mpaka 36 wana tatizo hili, Mziray na Kahabuka (2006). 

VITU HATARISHI VINAVYO PELEKEA TATIZO HILI:
1. Kumnyonyesha mtoto kila anapo hitaji baada ya kutimiza umri wa miezi sita.(breastfeeding at will after 6 months of age)

2. Tabia ya kulala usingizi huku chuchu ikiwa mdomoni mwa mtoto.
3. Kumpa mtoto maziwa ya chupa kupita kawaida, (extensive bottle feeding) au kumpa ili apate tu usingizi.
4. Matumizi ya vifaa vya vyenye utamu vya kunyonya mbadala ya chuchu viitwavyo Pacifiers.
5.Vinywaji vya sukari nyingi kwa mtoto ili tu kumfariji mtoto katika hali kama ya kulia.


Ni ukweli usiopingika kuwa watoto wanahitaji kupata maziwa kwaajili ya ukuaji mzuri; Na maziwa ya Mama ndiyo bora zaidi. Kwasababu hii shirika la Afya duniani WHO limetoa mstakabali kwamba watoto wanyonyeshwe maziwa ya mama tu(pekee) kwa muda wa miezi sita. Baada ya hapo vyakula vingine vinaweza tumika sambamba na maziwa ya mama.


Meno huanza kuota kinywani kwa mtoto akifikia umri wa miezi sita, hivyo sukari iliyomo katika maziwa inaweza sababisha meno kuoza katika kama tabia TANO hizo juu zitafanyika katika kumlisha mtoto.


Mfano mama kumuacha mtoto alale na chuchu mdomoni, mtoto akisinzia basi hawezi kumeza maziwa hivyo yatabaki tu mdomoni kwa muda mrefu hii hupelekea bakiteria kuitumia sukari iyo na kuzalisha asidi ambayo husababisha madini ya jino kuwa legevu na jino kutoboka.
Endelea kutufuatilia daktari mkononi kupata elimu juu ya matibabu ya tatizo hili. 

11 thoughts on “Ni mapema sana kwa mwanangu kuoza meno kiasi hiki!!.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show