Vidonge vya uzazi wa mpango na athari zake (Oral contraceptives).

Vidonge vya uzazi (oral contraceptives) ni moja kati ya dawa zitumiwazo sana na wanawake wa jamii ya kitanzania kwa nia ya kuzuia mimba ama kupunguza maumivu makali yatokanayo na hedhi

Dawa hizi zimekuwa zikitumiwa kimazoea au kutolewa na wahudumu wa afya bila kuangalia athari zake kama zitatumika kwa kipindi kirefu sana(zaidi ya miaka mitano 5 na hutokea kwa asilimia 1.6% kutokana na utafiti wa shirika la afya duniani WHO).

Yafuatayo ni madhara yatokanayona matumizi ya dawa za uzazi wa mpango kwa kipindi cha mda mrefu.

 1. Matatizo ya mfumo wa damu na moyo (Coronary heart diseases).
 2. Kupata Kiharusi (stroke).
 3. Uwezekano wa kupata saratani ya maziwa (breast cancer), Endometriosis pamoja na saratani ya ovari.
 4. Shinikizo kubwa la damu (hypertension).
 5. Magonjwa ya figo (acute kidney injury).
 6. Kuongezeka uzito kwa kiasi kikubwa.

 

Je ni nini natakiwa kufanya endapo natumia dawa hizi za uzazi wa mpango?

Endapo unatumia dawa hizi za uzazi wa mpango basi ni vyema ukafanya yafuatayo.

 1. Hakikisha una fanya mawasiliano na mhudumu wa afya ili kutambua ni kwa kiasi gani kuna ulazima wa kutumia dawa hizi ukiachana na njia nyingine za kuzuia mimba.
 2. Kuacha dawa hizi kwa mara moja (abrupt withdraw) haishauriwi na hivyo ni vyema kuwasiliana na mhudumu wa afya ili kujua ni lini na kwa sababu gani uache kutumia vidonge hivi vya uzazi.
 3. Kama bado hujaanza kutumia dawa hizi ni vyema kutoanza na kufanya njia nyingine rahisi za kuzuia mimba.

2 thoughts on “Vidonge vya uzazi wa mpango na athari zake (Oral contraceptives).

 1. Ahsante sana kwa makala yako nzuri. Lakini nina maswali yafuatayo.
  1. Unaposema “madhara yatokanayo na vidonge….yanapotumika kwa muda mrefu”, muda mrefu ndio muda gani hasa? Miezi 6? Mwaka 1? Miaka 10?

  2. Je vidonge vya uzazi wa mpango vina faida yeyote kwa mtumiaji?

  1. Asante Sana Hans Olomi kwa maswali mazuri na kuonyesha ufuatiliaji wa elimu hii kupitia Daktari Mkononi.
   Vitabu pamoja na majalada mengi ya uchunguzi yanaonesha uwezekano wa kupata athari hizi za mda mrefu kama mtumiaji anatumia vidonge hivi kwa muda wa zaidi ya miaka 10 kumi ingawa mara nyingine madhara huonekana mapema kutokana na sababu mbali mbali ambazo huchangia kutokea kwa athari hizo mapema.
   Vidonge vya uzazi vina faida nyingi tu ikiwamo
   1. Kuzuia mimba zisizotarajiwa
   2. Hutumika kutibu tatizo la maumivu wakati wa hedhi
   3. Hutumika kwa ajili ya matibabu ya saratani
   4. Pia hutumika kwa ajili ya kusaidia mzunguko wa homoni za kike (hormonal replacement therapy).

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show