Maambukizi ya kifua kikuu

Kifua kikuu ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na vimelea vya bakteria ajulikanae kama Mycobacterium tuberculosis. Kifua kikuu kwa kawaida kinaathiri mapafu, lakini huweza kuathiri pia sehemu nyingine za mwili kama uti wa mgongo, mifupa, moyo, ubongo na figo.

Kifua kikuu kinavyoambukiza
Kifua kikuu huambukizwa kwa njia ya hewa. Mtu mwenye uambukizo wa kifua kikuu ambaye bado hajaanza matibabu akikohoa, kupiga chafya, kuongea, kuimba au hata kucheka, vimelea vya kifua kikuu husambaa hewani na huweza kumuathiri mtu aliye karibu naye anapovuta hewa yenye vimelea hivyo. Baada ya vimelea vya kifua kikuu kuingia mwilini, mambo matatu huweza kutokea ambayo ni:
i. Uambukizo ambao hauonyeshi dalili
Mara nyingi vimelea vya kifua kikuu vikiingia katika mwili wa mtu aliye na hali nzuri ya lishe na afya, kinga ya mwili huweza kuviangamiza au kuvizuia vimelea hivyo kuzaliana. Hali hii ya uambukizo huweza kuonyesha dalili kidogo za muda mfupi au kutoonyesha dalili zozote kwani uambukizo unakuwa umezuiwa. Hali hii ya uambukizo ndio hutokea kwa watu
wengi.
ii. Uambukizo unaoendelea na kusababisha kifua kikuu
Uambukizo wa aina hii hutokea pale ambapo kinga ya mwili hushindwa kupambana na vimelea vya kifua kikuu vilivyoingia mwilini. Vimelea hivyo huzaliana na kuenea sehemu mbalimbali za mwili. Dalili huanza kujionyesha katika kipindi cha wiki sita hadi nane baada ya uambukizo.
Mara nyingi uambukizo wa aina hii hutokea kwa watu ambao hali zao za lishe na afya ni duni; kwa mfano watoto wachanga, watoto au watu wazima wenye utapiamlo na watu ambao kinga yao ya mwili imepungua.
iii. Uambukizo unaojitokeza baadaye
Uambukizo wa aina hii hutokea baada ya miezi au miaka michache baada ya kupata uambukizo ambao haukuonyesha dalili. Vimelea vya kifua kikuu huweza kuendelea kuishi bila ya kuzaliana na bila athari yoyote mwilini kwa muda mrefu. Kinga ya mwili inapodhoofika kwa sababu mbalimbali, vimelea huanza kuzaliana na kusababisha ugonjwa wa kifua kikuu.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show