Najuaje kuwa nina dalili za kifua kikuu?

Kifua kikuu usambaa kwa njia ya hewa, mtu anapovuta hewa yenye bacteria wanaosababisha kifua kikuu(Mycobacterium Tuberculosis) ,kinga ya mwili ufanya bacteria hawa wabaki katika mapafu ili kuzuia wasisambae sehemu nyingine za mwili kwa kuwazunguka na chembechembe hai za mwili. Panapotokea upungufu katika kinga ya mwili kwa mfano baada ya kupata magonjwa kama Upungufu Wa Kinga Mwilini (UKIMWI) ,saratani na hata matumizi ya dawa za kushusha kinga (Immunosuppressive drugs) kwa mfano cyclosporine ndipo ugonjwa huu huwa unaanza kuleta madhara ndani ya mwili na dalili uanza kuonekana. Zifuatazo ni dalili kuu za kifua kikuu

  1. Kukohoa makohozi au makohozi yenye damu kwa mda wa wiki 2 au zaidi
  2. Homa kali hasa wakati wa usiku
  3. Jasho kali wakati wa usiku
  4.  Kupungua kwa uzito
  5. Kuwahi kuchoka
  6.  Maumivu katika eneo la kifua
    Ni muhimu kumuona daktari kwa uchunguzi upatapo  dalili tajwa hapo juu.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show