Kwanini kwapa zangu zinakua na rangi nyeusi!?

Tatizo la rangi ya kwapa kubadilika na kuwa nyeusi zaidi ukilinganisha na sehemu nyingine za mwili limekua likiwaathiri watu wengi. Hali hii huweza kuleta fedheha, kuathiri aina ya nguo mtu anayotaka kuvaa na hata kushiriki kwenye shughuli mbalimbali kama kwenda ufukweni au sehemu nyingine za kuogelea.

Mtu yeyote anaweza kupata tatizo hili ingawa huwaathiri zaidi wanawake hasa wale wenye ngozi nyeusi. Hali ya weusi hutofautiana baina ya watu kwa sababu husababishwa na sababu tofauti; nyingi zikiwa zinatibika na wakati mwingine huwa ni kwa sababu ya tatizo la kiafya.

Sababu za hali hii
Sababu kuu zinazopelekea rangi ya ngozi ya kwapa kuwa nyeusi zaidi zipo tano

 1. Vinywele vigumu vinavyoota chini ya ngozi baada ya mtu kujinyoa kwenye kwapa hupelekea muonekano huu.
 2. Mkusanyiko/mlundikano wa seli za ngozi ya kwapa zilizokufa na kuleta muonekano huu.
 3. Matatizo ya ngozi kama pumu ya ngozi (eczema) au ‘hyperpigmentation’.
 4. Matokeo ya muingiliano kati ya viungo vinavyotengeza manukato (deodorants na antipersperants) na ngozi yako.
 5. Pia tatizo la kiafya linaloitwa “acanthosis nigricans” ambalo huambatana na kuwa na kiasi kikubwa cha insulini kwenye damu pale mtu anapokua na kisukari, uzito mkubwa au hali ya kurithi, kuwa na rangi nyeusi kwenye mikunjo ya ngozi hasa kwenye kwapa, shingoni na katikati ya mapaja.

Kuepukana na tatizo hili na kulitibu

 • Badala ya kunyoa vinyweleo kwa kutumia vifaa vya kunyolea unaweza ukafanya “waxing” au ukazinyofoa.
 • Kama tatizo ni seli zilizokufa au matatizo ya ngozi ni vizuri kuonana na daktari wa ngozi kwa matibabu sahihi.
 • Unaweza kubadilisha aina ya manukato unayotumia kama yanaingiliana na ngozi yako na kusababisha weusi.
 • Ukiwa mwenyewe nyumbani unaweza kujaribu njia hizi endapo rangi ya ngozi imeshabadilika;
  -Malimao: haya yana uwezo mkubwa wa usafishaji na kuua vijidudu. Kata kipande cha limao na usugue sehemu yenye weusi na baada ya dakika kadhaa osha na maji. Au
  -Viazi mviringo: hivi huwa na uwezo wa asili wa kuandoa rangi nyeusi. Kata kipande kisha sugua kwenye rangi nyeusi na ujisafishe kwa maji baada ya muda mchache. Au
  -Matango: haya yana uwezo asilia pia wa kutoa rangi nyeusi. Kata kipande na sugua mahali penye weusi kisha acha kwa lisaa limoja ndipo ujisafishe na maji.

14 thoughts on “Kwanini kwapa zangu zinakua na rangi nyeusi!?

 1. Asante dokta kwa maelezo mazuri,vipi njia hizi zinaweza kusaidia pia kwenye tatizo la kuwa na weusi katikati ya mapaja?! yaani zile sehemu ambapo chupi inapita?

  Lakini pia nauliza kama unaweza ukatuandikia na mada ya weusi kwenye mapaja. Hongera kwa kazi nzuri

  1. Asante sana Elizabeth
   Kuna baadhi ya sababu ambazo zinaingiliana hapo kama magonjwa ya ngozi, mlundikano wa seli za ngozi zilizokufa. Na kama sababu ni hizo basi njia nilizoeleza hapo juu zitatumika kuondoa tatizo hilo.
   Naomba nikuahidi pia kukuandalia makala itayoelezea zaidi Jumapili ijayo.
   Karibu tena Daktari Mkononi

  1. Asante Clarissa kwa swali zuri
   Basi naomba nikuahidi kwamba nitaandaa makala ya kukuelezea tatizo hili kwa urefu hapo Jumapili ijayo kwa sababu sababu huwa ni nyingi na mojawapo ikiwa ni maambukizi ya bakteria.
   Karibu tena Daktari Mkononi

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show