Yajue matumizi ya Viagra

Ndoa na mahusiano mengi huharibika kwasababu jinsia ya kiume kushindwa kukidhi hitaji kuu la mwili hivyo husababisha ulazima wa kwenda kujiridhisha nje ya mahusiano hayo (kuchepuka) au pia kuvunjika kwa mahusiano mengi. Mwanaume hushindwa kusimamisha uume wake na kuumudu, tatizo ambalo husababisha mawazo (stress) na kuathiri kujiamini kwake.

Kwanini nnapata tatizo hili?

Matumizi ya pombe, magonjwa kama kisukari, matumizi ya tumbaku, mawazo(stress), huzuni(depression), wasiwasi(anxiety) nk. ndio viaelelezo vikuu vya tatizo hili.

Jinsi gani ninaweza kujikinga na tatizo hili?

Kufanya mazoezi, kupunguza msongamano wa mawazo, huzuni na wasiwasi.

Dawa gani itumike?

Sildenafil citrate al maarufu Viagra.

Ilivumbuliwa kwa matibabu ya magojwa ya moyo na angina ila zikaonekana kutibu magonjwa hayo kwa kiasi na kuongeza nguvu za kiume zaidi kama madhara ya kutumia dawa hiyo. Matumizi yake yalibadilika rasmi.

Hutumika kusimamisha uume kwa mwanaume ambaye ameshapata mihemko. Haitumiki kuleta mihemko. Mihemko husababisha kemikali za ndani ya mwili kuifanya mishipa ya maeneo mbalimbali ya mwili kutanuka ikiwemo mishipa ya uume na kuruhusu damu ya kutosha kupita, hivyo dawa hii hufanya mishipa hiyo kutanuka kwa muda mrefu zaidi.

Hutibu matatizo ya uume kutokusimama kwa wanaume tuu na haijaonekana kuonesha athari ya aina yoyote kwa wanawake na wanaume wasio na tatizo hilo.

Kuna madhara yoyote yaambatanayo na utumiaji wa dawa hii?

 • Kichwa kuuma.
 • Kiungulia.
 • Pia inasemekana kuwa inaweza kusababisha uume kusimama kwa muda mrefu (prolonged erectionambayo huweza kusababisha madhara kwenye uume.
 • Kupata shida kuona (kuona ukungu au kuona kila kitu rangi ya bahari, buluu).
 • Pua kuziba.
 • Unyeti wa mwanga (sensitivity to light).
 • Na pia inaweza ikaongeza mapigo ya moyo na kusababisha moyo kuzidiwa na kazi yake na kupelekea kifo.

Watu gani wasitumie dawa hizi?

 • Wanoatumia dawa za presha zinazotanua mishipa ipitishayo damu (jamii ya naitriki oxaidi).
 • Wenye matatizo ya figo na ini.
 • Wenye matatizo ya presha ya damu kushuka.
 • Watu waliowahi kupata kiharusi.
 • Watu wenye maambukizi ya virusi vya UKIMWI wanaotumia dawa zinazozuia protease (protease inhibitors), jamii ya lopinavir, atazanavir, ritonavir nk.

Matumizi ya dawa hii yanapaswa kua na uangalifu wa hali ya juu na hushauriwa kutumika endapo tu kama imeshauriwa na daktari wako. Vijana wengi huitumia kwa matumizi yasiyosahihi na hivyo hutumika kama madawa ya kulevya. Kwenye michezo pia imebainika kua husaidia kuongeza misuli ya wanariadha na kuongeza ufanisi wao katika michezo.

15 thoughts on “Yajue matumizi ya Viagra

 1. Ujumbe mzuri, ila ingekuwa vizuri zaidi kama watu wangeelimishwa jinsi ya kujikinga na huko kutoshindwa kujamiiana ili wasifikie kutumia hizo viagra.

 2. Habari yako Daniel,
  Ahsante kwa swali zuri, viagra ni dawa ambayo hupatikana kwenye maduka ya dawa (Pharmacy). Pia upatikanaji wake huhitaji cheti cha daktari. Bei yake huanzia 1500-2500, hutegemeana. Pia hakikisha unapewa maelekezo juu ya matumizi na madhara yake.
  Endelea kua nasi daktari mkononi kwa elimu zaidi juu ya afya.

  1. Habari yako ndugu Simion. Mabadiliko hayatokei kwa kutumia dawa peke yake. Inapaswa kuzingatia mambo kadha wa kadha ili kuweza kutatua tatizo hili. Wasiliana nasi kupitia nambari yetu ya simu ya mkononi 0762952137 kwa msaada binafsi zaidi. Ahsante na endelea kufurahia huduma yetu ya bure ya daktarimkononi.

 3. Habari Dr Belinder pole na majukumu.Mimi ningependa kujua Kama ni Athari gani itatokea kwa mtu kutokufanya tendo la ndoa kwa muda mrefu?

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show