Chanjo kwa watoto

Ukweli kuhusu chanjo za watoto.

  1. Kulingana na takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), chajo zinazuia takriban vifo million mbili hadi tatu kila mwaka duniani.
  2. Chanjo ndiyo njia salama zaidi ya kumkinga mtoto dhidi ya magonjwa ambukizi yanayoweza kumlemaza ama kumuua. Baadhi ya magonjwa ni kama:kifaduro(whooping cough),ukambi(measles),pepopunda(tetanus),kifua kikuu(T.B) na ugonjwa wa kupooza(polio).

3.Ni vizuri mtoto kupata chanjo ata kama unadhani hayuko katika hatari ya       kuambukizwa.Hii ni kwa sababu magonjwa kama ukambi na ugonjwa wa kupooza yanaweza  kuimbuka kwa ghafla katika jamii na kuhatarisha afya ya mtoto yeyote aliyekosa kuchanjwa.

  1. Chanjo nyingi kwa pamoja ni salama na zina manufaa..Vilevile kupewa chanjo nyingi kwa wakati mmoja huhakikisha hakuna kupoteza wakati na rasilimali.
  2. Watoto wakiacha kuchanjwa magonjwa yaliyopotea ama kukua nadra yanaweza kurudi tena na kuleta maafa makubwa kiafya duniani.

 Dhana potovu kuhusu chajo za watoto.

  • Baadhi ya chanjo zinaweza kulemaza watoto-huu ni uongo mtupu.Shirika la Afya Duniani (WHO) limehakikisha kuwa hamna chanjo iliyo na madhara inatumiwa popote duniani.
  • Ni vizuri kukawia kabla ya kumuanzisha mtoto chanjo-si jambo za busara kuchelewa kumpeleka mtoto chanjoni kwani huku nikuhatarisha maisha yake na ya wengine.
  • Ukimnyonyesha mtoto haina haja ya chanjo-maziwa ya mama hayatoshi kamwe kumkinga mtoto dhidi ya magonjwa hatari ambukizi.
  • Haina haja kumpeleka mtoto kuchanjwa ikiwa watoto wengi katika jamii walishapata chanjo-hii ni fikra ambayo haifai asilani.Ni wajibu wa kila mzazi kuhakikisha mtoto wake amechanjwa wala si kutengemea vitendo vya wazazi wengine.Isitoshe,kinga ya kweli dhidi ya magonjwa ambukizi hupatakina tu kila mtoto akichanjwa kibinafsi.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show