Tatizo la Usonji (autism) kwa watoto

Usonji ni tatizo linaloathiri uwezo wa mtoto kuwasiliana na watu wengine, kujitenga na watu, na kuwa na tabia ya kurudia rudia kitu mara nyingi. Mtoto huwa na tabia za kipekee na kuonekana tofauti na watoto wengine.

Tatizo hili humpata mtoto mmoja kati ya watoto 160 duniani kutokana na utafiti uliofanyika na shirika la afya duniani (WHO). Kutokana na jamii kutokua na uelewa wa kutosha juu ya tatizo hili, watoto hawa huishiwa kuteseka kwa kutokupata matibabu na huduma sahihi hata ikapelekea baadhi yao kupelekwa kwa waganga sababu ya Imani potofu au kutengwa kabisa.

Chanzo cha tatizo hili hakijajulikana bado lakini kuna sababu hatarishi zinazoweza kupelekea tatizo hilo kama

Mama kupata mtoto wa kwanza katika umri mkubwa yaani Zaidi ya miaka 35

Mama mjamzito kuwa na kisukari kipindi cha ujauzito

Dalili zake

Dalili za ugonjwa huu huonekana pale mtoto anapofikisha umri wa kuanza kuelewa na kuzungumza kama watoto wengine

 • Kushindwa kuzungumza maneno yanayoeleweka hivo kushindwa kueleza hisia zake au kitu anachokitaka. Mtoto hurudi rudia maneno
 • Kushindwa kuonyesha ishara za kimwili za mawasiliano kama kupunga mkono, ishara za usoni(facial expression)
 • Kuwa mzito wa kuelewa mambo ukilinganisha na watoto wengine lakini akielewa anakuwa na uelewa mkubwa wa hicho kitu kimoja kuliko watoto wengine.
 • Kuwa na tabia za kujirudia rudia, mfano kupenda kucheza mchezo mmoja kila siku, tabia zinazochukua mda mwingi kam kupanga vitu kwa mpangilio maalumu mara kwa mara
 • Kujitenga na wenzake. Hushindwa kujichanganya na wenzake katika michezo na kubadilishana mawazo
 • Kushindwa kuangalia watu machoni
 • Kuepuka kelele, kushikwa. Hii hutokana na kuathirika kwa jinsi ya akili inavyotuma na kupokea ujumbe kutoka kwenye milango ya fahamu.

Tatizo hili halina tiba ya moja kwa moja bali watoto hawa wana shule maalumu kwa ajili ya kuhudumia mapungufu yao katika mawasiliano, lugha, na tabia zao.

Ikumbukwe kuwa watoto wenye tatizo hili hawana ulemavu katika kila kitu bali huwa na uwezo wa kipekee na mkubwa kuliko wengine katika kile wakipendacho kukifanya kwa kujirudia rudia, mfano mtoto mwenye usonji anaweza kuwa na uwezo mkubwa kwenye somo la hesabu na kushindwa masomo mengine yote.

Watoto hawa pia wanakua na uwezo mzuri endapo malezi na mazingira ya malezi nyumbani yatakua mazuri.

Muone daktari uonapo dalili hizi kwa mtoto wako pale anapofikisha umri wa kuweza kuwasiliana.

 

7 thoughts on “Tatizo la Usonji (autism) kwa watoto

 1. Shukran daktari kwa elimu nzuri.
  Pia wengine wakita kuelewa kuhusu autism waangalie tamthilia iitwayo the good doctor.
  Kazi njema.👏

  1. Halitibiki moja kwa moja ila kuna huduma maalumu wanapata katika shule maalumu, shule hizo zina walimu wanaowafanyia mazoezi ya lugha(speech therapy), mazoezi ya kutumia viungo vyao ipasavyo (physiotherapy) ili kuwasaidia waweze kumudu maisha ya kila siku na jamii inayowazunguka.

 2. Asante kwa nondo daktari,
  hivi kwa nini tatizo linawapata watoto wanaozaliwa katika umri mkubwa wa mama ( 35 and above)?

 3. nimeelewa kile ulicho kifundisha hapa tunahitaji elimu zaidi kufikia wana nchi wetu wengi hasa wa vijijini zaidi kwa 7bu wengi huwa tunakimbilia kusema tumelogewa

  1. Asante kwa kutambua mchango wetu..karibu Daktari mkononi kwa elimu zaidi. Kuhusu kufikia watu vijijini kuna mfumo wa simu ambao mtu yoyote popote alipo anaweza wasiliana nasi kwa ujumbe au kupiga simu kupitia namba 0688 636 717 au 0762 952 137

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show