Mshtuko wa moyo

Mshtuko wa Moyo
Baadhi ya wakati mshituko wa moyo hutokea kwa dalili zilizo wazi na kwa haraka sana. Lakini mara nyingi mshituko wa moyo hutokea polepole huku mtu akipata maumivu ya wastani na kutokujisikia vyema.
Mara nyingi watu wanaopatwa na hali kama hiyo huwa hawana uhakika na kile kinachotokea na husubiri kwa muda mrefu kabla ya kuomba msaada au kumuona daktari.
Zifuatazo ni dalili ambazo hutokea pale mtu anapopatwa na mshituko wa moyo.

1) Maumivu katika kifua: Mtu huhisi kana kwamba kifua kinambana, kimejaa na kinauma.
2) Maumivu katika sehemu za juu za kiwiliwili: Mtu huhisi maumivu sehemu za mikono, mgongo, shingo, taya na tumbo.
3) Kukosa pumzi au kushindwa kupumua
4) kizunguzungu
5) Moyo kwenda mbio au kwa ibara nyingine mapigo ya moyo kutokea kwa kasi zaidi kuliko kawaida.
Unashauriwa iwapo utajisikia maumivu ya kifua, hasa pamoja na mchanganyiko wa moja ya dalili hizo usisubiri na haraka wasiliana na kituo cha afya ili upatiwe msaada, au elekea haraka hospitali mwenyewe. Muda unaofaa wa kutibiwa mshituko wa moyo ni saa moja tangu wakati wa kutokea hali hiyo. Kutibiwa mapema dalili za mshituko wa moyo hupunguza hatari ya kuharibika seli za moyo. Hata kama huna uhakika dalili unazohisi ni za mshituko wa moyo au la, ni bora umuone daktari na ufanyiwe uchunguzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show