Jifunze unywaji sahihi wa pombe.

Kwa ajili ya afya njema na utimamu wa akili inashauriwa kunywa pombe kwa kiasi au ikiwezekana kutokunywa kabisa kwa wale wasiotumia, hii ni kwa sababu hasara za unywaji wa pombe ni nyingi sana ukilinganisha na faida zake.

Kwanini ninywe kwa kiasi?
Hii ni kwa sababu unywaji wa pombe wa kiasi una faida nyingi sana, zikiwemo;
– Kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo kama vile shinikizo la damu (hypertension).
-Kupunguza hatari ya kupata kiharusi (stroke).
-Pia magonjwa kama vile kisukari na homa ya ini yanaweza kuepukika kwa kunywa pombe kwa kiasi.

Unywaji wa pombe wa kiasi ni upi?
Kulingana na tafiti mpya, inashauriwa kutumia pombe vizio viwili (2 units) au pungufu kwa siku. Kwa hiyo haishauriwi kuzidisha vizio 14 (14 units ) kwa wiki. Hii ni kwa wote, wanaume na wanawake.
Ni vyema kutokunywa pombe kabsa kwa siku nyingi zaidi katika wiki ambayo itakufanya ujiweke mbali na magonjwa ya muda mrefu yatokanayo na pombe, ajali na majeraha yatokanayo na ulevi wa kupindukia

Utapataje kujua hivyo vizio (units) vya pombe;
(ujazo wa pombe×asilimia za kilevi) gawanya kwa 1000

Jali afya yako, kunywa pombe kwa kiasi.

2 thoughts on “Jifunze unywaji sahihi wa pombe.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show