Jinsi gani tunaweza kujiepusha na madhara ya magonjwa ya moyo Kama mshtuko wa moyo

Kwa wale ambao tayari wameshapatwa na ugonjwa huu pia wanashauriwa kuendelea kutumia dawa walizopewa hospitalini lakini pia kubadilisha mienendo ya maisha yao ili kuzuia kupatwa tena na mshituko wa moyo katika siku zijazo.
Kwa wale ambao mshituko wao wa moyo umesababishwa na magonjwa mengineyo waliyonayo kama matatizo mengine katika moyo au maradhi tofauti, wanatakiwa kutibiwa maradhi hayo.
Lakini kwa ujumla tunaweza kujiepusha kupatwa na ugonjwa huo kwa
1. kutovuta sigara

2. kudhibiti hali nyinginezo kama shinikizo la damu, ongezeko la mafuta ya kolestroli mwilini na kisukari

3. kuushughulisha mwili kila mara na  kufanya mazoezi

4. kupata lishe bora,

5. kupunguza uzito uliopindukia wa mwili

6. kupunguza ua kujiepusha na wasiwasi pamoja na msongo wa mawazo.

Daima tuzilinde afya zetu!

1 thought on “Jinsi gani tunaweza kujiepusha na madhara ya magonjwa ya moyo Kama mshtuko wa moyo

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Privacy Preference Center