Mpangilio mbaya wa meno (malooclusion).

Malocclusion ni hali ya kuwa na mpangilio usio sahihi wa meno katika  taya la juu au/na chini ,au kukosa uwiano yanapokutana  sawasawa na ule uitwao wa kawaida (normal occlusion). Mpangilio usio sahihi hujumuisha mambo mbalimbali kama; meno ya juu au ya chini kuwa mbele pasipo kawaida, meno kukosa nafasi (crowding), meno kuota juu ya meno mengine au kujipanga pasipo sahihi, nafasi kubwa kati ya jino na jino (spacing), meno ya juu kutokukutana na meno ya chini na kusababisha uwazi (open bite) na kusababisha  kukosekana kwa uwiano kati ya taya la juu na la chini.

Kuna sababu mbalimbali zinazoweza kusababisha  kukosekana kwa uwiano huo. Sababu  hizo ni pamoja na;

  • Sababu za kurithi (hereditary) ambapo mtu hurithi meno makubwa kutoka kwa mzazi mmoja na taya dogo kutoka kwa mzazi mwingne. Hali hii hupelekea mtu kuwana taya dogo lisiloweza kutosheleza ukubwa wa meno yake  na kusababisha meno kukosa nafasi (crowding) na/au kuota vibaya.
  • Sababu za kimazingira na tabia mbalimbali kama kunyonya vidole kwa muda mrefu, kunyonya ulimi (tongue thrusting), kupumua kwa kutumia mdomo (mouth breathing) au kupoteza mapema kusiko kawaida kwa meno ya utotoni (early loss of primary dentition). Sababu  hizi huwa na athari kubwa katika kipindi meno ya ukubwani yanapoota na kusababisha yaote katika mpangilio usio sahihi.

Meno yaliyo katika mpangilio usio sahihi yanaweza kusababisha vitu vifuatavyo;

  • Kuharibu muonekano wa mtu na kupunguza kujiamini (esthetics and confidence)
  • Huongeza uwezekano wa kupata magonjwa ya fizi na meno kutoboka kwani meno yaliyo katika mpangilio mbaya huleta shida katika kuyasafisha.
  • Hupunguza uwezo wa kufanya kazi kama kutafuna kwani hayapo katika uwiano sahihi .
  • Kushindwa kutamka baadhi ya maneno vizuri hasa yenye herufi  S na V.
  • Kujiumiza mara kwa mara kinywani meno yanapokutana (deepbite).

Je nifanye nini nigunduapo tatizo hili? Ni rahisi sana,muone mtaalamu wa  afya ya kinywa na meno kwa ajili ya uchunguzi, ushauri na matibabu.

2 thoughts on “Mpangilio mbaya wa meno (malooclusion).

  1. Asante doktakwa maelezo je mtu mzima anaweza kupanga meno yake yakakaa vizuri je inachukua muda gani hayo matibabu?

    1. asante kwa swali zuri. Mtu mzima anaweza kupanga meno na yakakaa vizuri, tofauti ni muda atakaotumia kwa ajili ya matibabu hayo. muda utakuwa mrefu zaidi tofauti na mtoto. muda huweza kuanzia mwaka na nusu mpaka miaka mitatu kutokana na usugu wa tatizo.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show