Faida za kutumia limao

Mara nyingi huwa tunafikiri limao ni kwa kina mama wajawazito tu. Lakini limao linamanufaa hata kwa watu wengine pia, fuatilia faida za kutumia maji ya limao.

1: Inaleta uafadhali baada ya kuvimbiwa na kulainisha choo.
Maji ya limao husaidia katika kulainisha choo hivyo unaweza kutuitumia endapo unashida kwenye kupata choo au unapokua umevimbiwa.
2:Hupunguza homa
Endapo mtu anakua ana homa inayotokana na mafua au kikohozi maji ya limao husaidia kupunguza homa.
3: Huzuia kutoka damu puani
Inapotokea damu inatoka puani unaweza kutumia maji ya limao kuzuia damu. Chukua pamba kidogo iloanishe na limao kisha weka puani.
4: Kupunguza uzito
Kama mtu anataka kupunguza uzito anashauriwa kunywa juisi ya limao. Chemsha maji ya limao na uongeze asali kisha yatumie mara kwa mara.
5: Afya ya kinywa
Maji ya limao husaidia kupunguza harufu mbaya mdomoni, kwa kutusugulia kipande kidogo cha ndimu kwenye meno inaweza kuondoa harufu mbaya.
Lakini inatakiwa kuwa makini unaposugulia limao, ukisikia maumivu acha mara moja na umuone daktari
6: Hutumika katika kutunza nywele
Maji ya limao hutumika kupunguza mba, kupukutika kwa nywele na huzing’arisha nywele.
7: Utunzaji wa ngozi
Limao husaidia kupunguza maumivu yanayotokana na kuungua na jua, chunusi na pia husifika kwa kupunguza makunyanzi ya ngozi. Kunywa juisi ya Limao ambayo imechanganywa na asali husaidia ngozi kuwa yenye afya.

2 thoughts on “Faida za kutumia limao

  1. Asante,eti ni kweli malimao yanakata tumbo?! yani ukinywa juisi ya limao unaweza kupunguza tumbo,mnaona hapa umesema uzito

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show