Muda gani unafaa kunywa maji?

Kila mtu anajua kuwa ni muhimu kunywa maji, ili mmeng’enyo wa chakula uendelee vizuri, kutunza ngozi na kuuchangamsha mwili. Lakini huwa tunashindwa kunywa maji kiasi kinachohitajika.

Inashauriwa kunywa maji glasi nane kwa siku, lakini je, unafahamu uni muda gani unafaa kwa ajili ya kunywa maji? Jaribu kufuatisha kunywa maji katika muda huu na itakua rahisi kunywa maji ya kutosha.
1: Baada ya kuamka
Kunywa glasi moja ya maji baada ya kuamka ilikuvichangamsha viungo vya mwili.
2: Kabla ya chakula
Kunywa glasi moja ya maji nusu saa kabla ya kula, hii itasaidia katika mmeng’enyo wa chakula. Epuka kunywa maji kipindi cha chakula, kwani maji yatazifanya kemikali za mmeng’enyo kupooza na kutofanya kazi vizuri. Unaruhusiwa kunywa maji saa moja baada ya kula.
3: Kabla ya kuoga
Kunywa glasi moja ya maji kabla ya kwenda kuoga, hii itasaidia kuweka shinikizo la damu vizuri kabla ya kuoga
4: Kabla ya kulala
Kunywa glasi ya maji kabla ya kulala hii itafidia maji yatakayopotea kipindi cha kulala.
5: Kabla na baada ya mazoezi
Inashauriwa kunywa maji kabla ya kuanza mazoezi na baada ya kumaliza mazoezi au kazi nzito iliyosababisha kutoka jasho. Hii itafidia maji yaliyopotea kutoka mwilini.

3 thoughts on “Muda gani unafaa kunywa maji?

 1. Kuna mkanganyiko kidogo..kwa mujibu wa hii article, kiasi cha maji ni glass nane…lakini kulshakuwa na article nyingine ambayo inaelezea jinsi ya kucalculate kiwango cha maji kwa siku…so i guess inabd iwekwe sawa ijulkane ipi ni ipi kusiwe na mkanganyiko

 2. Kwanza niwapongeze kwa kazi nzuri, lakini;
  Napata shaka kuamini usahihi wa taarifa zilizotolewa katika post hii, ndio maana niliwahi kuomba mtoe Marejeo(references) mnapotoa taarifa.
  Nanukuu mmesema “Epuka kunywa maji kipindi cha chakula, kwani maji yatazifanya kemikali za mmeng’enyo kupooza na kutofanya kazi vizuri”. Hii si sahihi

  PH ya kemikali zinazomengenya chakula inarange kati ya 1-4. Ili kubadilisha, pH hii inahitaji mtu anywe angalau anywe litre 45 za maji ili kupoozesha kemikali zinazomeng’enya chakula, yaani kupandisha pH juu ya nne. Kwahiyo mtu hata anywe glass ngapi wakati wa chakula, hawezi kufikisha kiwango kinachoweza kupoozesha kemikali.

  Pia tafiti mbalimbali zimefanywa na zimeonyesha vimiminika, havibadilishi kasi ya mmenngenyo wa chakula kwa kiwango kikubwa.
  Rejea: http://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/371939
  http://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/7083695
  http://www.mayoclinic.org/healthy-lifestyle/nutrition-and-healthy-eating/expert-answers/digestion/faq-20058348
  http://water.usgs.gov/edu/qa-solvent.html
  https://fxnutrition.com/water-with-meals/

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show