Zijue faida za maziwa ambazo hujawahi fikiria

Sio utamaduni wa familia zetu za kitanzania kunywa maziwa mara kwa mara. Na mara nyingi sio kwa kuwa hatuna uwezo wa kununua ila ni kwasababu pengine hatufahamu faida nyingi za maziwa. Maziwa ya ng’ombe yana virutubisho vingi ikiwemo maji ,na madini mengi kama calcium na potasiamu na hata vitamini.

Je, ni faida zipo zinatupasa tujenge tabia ya kunywa maziwa?

  • Maziwa na afya ya moyo; kwa kuwa maziwa yana madini ya potassium hutanua mirija ya damu na hivyo kuepusha matatizo ya shinikizo la damu na kiharusi.
  • Maziwa kwenye saratani; uwepo wa vitamin D kwenye maziwa husaidia katika ukuaji wa seli za mwili na hii husaidia kupunguza hatari ya ukuaji wa seli za saratani. Hivyo kupunguza hatari ya saratani hasa ya utumbo mkubwa.
  • Maziwa na tatizo la msongo wa mawazo; husaidia katika uzalishaji wa homoni ya serotonini inayohusika na usingizi,hamu ya kula na hata hali ya furaha kwa uwepo wa vitamin D katika maziwa
  • Maziwa na afya ya meno; hasa kwa watoto maziwa hutoa ulinzi imara kwa meno yao kwa kuimarisha sehemu ya juu kabisa ya jino na kuepusha meno kuoza na kufanya fizi kuwa imara.
  • Maziwa katika kujenga mwili; kwa kuwa maziwa yana kiwango kikubwa cha protini yanasaidia pia katika kujenga mwili na hii kuyafanya kuwa yenye faida hata kwa wanamazoezi.
  • Maziwa na mifupa; kwa kuwa maziwa yana madini ya calcium ambayo ni muhimu pia kwa ukuaji wa mifupa na kuiimarisha na kuepusha urahisi wa kuvunjika kwa mifupa.

Ni vyema kujenga tabia ya kunywa maziwa hata mara chache kupata faida za kiafaya. ni bora kinga kuliko tiba.

2 thoughts on “Zijue faida za maziwa ambazo hujawahi fikiria

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show