fangasi za kwenye mdomo.

 

Tatizo la fangasi mdomoni linatokana na kukua kwa fangasi aina ya candida albicans ambao husababisha muwasho na hali kama ya kuungua mdomoni,kusikia ladha kama ya chumaย  ikiambatana na weupe fulani kwenye mdomo au ulimi ambao unabanduka ukiukwangua.

Zifuatazo ni sababu zinazoweza kupelekea kupata fangasi mdomoni.

 • Matumizi ya muda mrefu ya dawa za kuua bakteria(antibiotics)
 • Kuwa na tatizo la kukaukiwa na mate mdomoni(xerostomia)
 • Ukosefu wa baadhi ya virutubisho na madini mwilini kama madini chuma,na vitamin kadhaa.
 • Kuwa mjamzito,wazee wenye umri mkubwa,au watu wenye utapiamlo.
 • Matumizi ya tumbaku,ugoro na kuvuta sigara
 • Kuwa na meno bandia ambayo hayakai vizuri mdomoni(Ill fitting dentures)
 • Kushiriki ngono kwa njia ya mdomo(oral sex) na mtu ambaye ana fangasi kwenye via vya uzazi.
 • Kuwa na magonjwa sugu kama kisukari hasa kwa wale ambao hawafatilii vizuri matibabu ya ugonjwa huu.
 • Kuwa na magonjwa yanayoshambulia kinga ya mwili kama virusi vya UKIMWI
 • Kufanyiwa matibabu ya mionzi(RADIATION THERAPY)
 • Watoto wachanga wanaweza kuwa na fangasi hizi ambazo huonekana kama utando mweupe mdomoni mara nyingi huwa wanapona wenyewe,lakini pia inawezekana kabisa wakapata fangasi kutoka kwenye ziwa la mama kama lina maambukizi.

Endapo una tatizo hili fanya yafuatayo.

 • Endelea kufanya usafi wa kinywa vizuri kwa kupiga mswakiย  angalau mara mbili kwa siku.
 • Tunza vizuri meno yako bandia kama ulivyoelekezwa.
 • Unaweza kujaribu kusukutua na maji ya uvuguvugu yenye chumvi kwa siku tatu.
 • Ongeza matumizi ya vyakula aina ya maziwa mtindi na yoghurt hizi husaidia kupambana na fangasi.Pia kula mlo kamili(balanced diet)
 • Epuka tabia zinazoweza kukusababishia kupata fangasi mdomoni kama zilivyoelezwa hapo juu.
 • Nenda hospitali kupatiwa msaada wa kitaalamu kutoka kwa wataalamu wa kinywa na meno au madaktari bingwa wa koo,pua na masikio(ENT specialists).

Kuwa na fangasi kwenye mdomo kunaweza kusababisha mdomo kutoa harufu mbaya na hata kubadilisha ladha ya chakula uonapo dalili au kuhisi kuwa una fangasi mdomoni usisite fika hospitali kupatiwa msaada kwani fangasi hizi zinaweza kusambaa na kufika maeneo mengine hasa kwenye koo la chakula hivo kusababisha matibabu kuwa shida zaidi,wahi mapema kupata matibabu.

 

 


Flaviana Nyatu DDS 5 ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ

A happy and passionate dental surgeon.

All author posts

Privacy Preference Center