Ifahamu mimba zabibu (sehemu B)

Baada kujifunza maana ya mimba zabibu na baadhi ya vihatarishi, katika sehemu hii tujifunze kuhusu dalili za mimba zabibu na nini mama afanye aonapo dalili hizi.
Kama ilivyosemwa hapo awali, mimba zabibu huwa na dalili za mwanzo za mimba kama vile kichefuchefu na kutapika, lakini kichefuchefu na kutapika huku HUZIDI KAWAIDA, HAKUWEZI KUVUMILIKA. Kitaalamu hali hii huitwa hyperemesis gravidarum. Hali hii huweza kumpelekea mama kushindwa kula kabisa, kuishiwa maji mwilini, kupata madhara ya kupungukiwa madini mwilini kama potassium.
Mbali na hapo dalili zingine huweza kuwa;
•Kutokwa damu ukeni, hii huweza kuwa matone tu au damu nyingi.

•Mama kuona akitoka vitu venye mfano wa zabibu au vinyama kutoka ukeni

•Maumivu ya tumbo

•Baadhi ya wanawake hasa wale wenye complete mole huweza kupata dalili zinazotokana na kuzidi kwa homoni iitwayo thyroid. Dalili hizi ni kama wasiwasi uliopitiliza, mapigo ya moyo kwenda mbio, kuhisi joto kupita kiasi, uchovu uliokithiri.

•Mama pia huweza kugundulika kuwa na presha kubwa (mgandamizo mkubwa wa damu) na hali hii hujitokeza mapema sana katika ujauzito. Wengine kupata dalili hii katika wiki 13 za mwanzo.

• Kutokusika kwa mapigo ya moyo ya mtoto-hali ambayo mama atapewa taarifa kliniki au mama mwenyewe kushindwa kusikia mtoto akicheza tumboni. Kawaida mtoto huanza kucheza tumboni kuanzia mimba yenye umri wa wiki 16-25

Uchunguzi zaidi kwa mama mwenye dalili zozote kati ya hizi tajwa hufanyika katika kituo cha afya na wataalamu, baadhi ya uchunguzi huu huusisha wataalamu kupima kiwango cha homoni iitwayo Beta-HCG ambayo huwa juu sana kwa mama mwenye mimba zabibu. Kipimo kingine ni picha ya tumbo yaani ultrasound.
Matibabu ya mimba zabibu ni hutolewa kwa uvimbe huu kutoka katika mji wa uzazi na kusafishwa na wataalamu wenye ujuzi wa kufanya hivyo. Baada ya hapa mama huendelea na kipimo vya homoni ya Beta-HCG kuona maendeleo yake. Asilimia kubwa ya wanawake hawa hurudia hali ya kawaida, ingawa iko asilimia ambayo huweza kupata saratani katika mji wa uzazi.
Pia inashauriwa mama asipate ujauzito katika kipindi hiki cha uangalizi. Kipindi hiki kisipungue mwaka mmoja.

Kupoteza mimba zabibu kuna athari kisaikolojia kama ilivyo kupoteza mimba ya kawaida. Hivyo familia na jamii kwa ujumla inapaswa kumpa mama faraja ili arudie hali yake ya kawaida

 

Reviewed by Dr. Msiry

References.
1. MedlinePlus [Internet]. Bethesda (MD): National Library of Medicine (US); [updated 2006 Feb 21]. Pregnancy Loss; [updated 2006 Feb 22; reviewed 2006 Feb 7; cited 2006 Feb 22].

http://www.nlm.nih.gov/medlineplus/pregnancyloss.html

2. Current Obstetric & Gynecologic Diagnosis & Treatment-Ninth Ed. DeCherney, Alan H., et al, Ch. 50.

2 thoughts on “Ifahamu mimba zabibu (sehemu B)

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show