Warts ni nini?
Warts ni viuvimbe vidogo (Vinyama) vinavyosababishwa na virusi aina ya HPV (Human papilloma virus)
Viuvimbe hivi vinaweza kuota kimoja au kwa wingi. Na hutokea sehemu mbalimbali kama sehemu za siri za wanawake na wanaume, sehemu ya haja, mdomoni na sehemu nyingine tofauti.
Leo tutaongelea hasa vinavyotokea sehemu za siri za wanawake.
Uwezekano wa kupata ugonjwa huu kwa wanawake ambao wameshaanza kufanya tendo la ndoa ni zaidi ya asilimia 50% angalau mara moja katika maisha yao.
Ugonjwa huu huwapata wanawake walio kati ya umri wa miaka 17-33. Asilimia 75% ya watu ambao wamejamiana na mtu mwenye ugonjwa huu huanza kuonyesha dalilo ndani ya miezi mitatu.

Nitaambukizwaje ugonjwa huu?
Ugonjwa huu huambukizwa kwa mgusano wa mwili kwa mwili na hivyo mwanamke hupata ugonjwa huu pale anaposhiriki tendo la ndoa na mwanaume aliye na ugonjwa huu bila kinga.
" Dalili za ugonjwa huu ni zipi?
•Kupata viuvimbe vyenye rangi ya ngozi ( muda mwingine huwa kama vinyama) katika sehemu za siri.
•Vinaweza vikawa vinawasha na kukuletea maumivu.
•Kutokwa na ute usio wa kawaida ukeni.
•Kutokwa na damu baada ya kushiriki tendo la ndoa.


Nani yupo katika hatari zaidi ya kupata ugonjwa Huu?
•Wanawake walio chini ya miaka 30.
•Wanawake wanaovuta sigara.
•Wanawake wenye upungufu wa kinga mwilini.
je, Najiepushaje?
•Kutumia kinga wakati wa kujamiana
•Kupata chanjo dhidi ya virusi hivi.
•Kuacha kuvuta sigara.
•Epuka kuvigusa gusa.


Nifanye nini pale nipatapo warts?
Unashauriwa kumuona daktari ili kupatiwa matibabu ya genital warts,
Ifahamike kuwa hakuna matibabu ya moja kwa moja ya ugonjwa huu kwa sababu unasababishwa na virusi na kawaida virusi huwa havina tiba ya moja kwa moja,hivyo matibabu hufanya ili kuondoa kero zinazosababishwa na ugonjwa huu Kwa mfano muwasho na maumivu pia kupunguza ukubwa wa hivi vinyama.
Ifahamike kuwa vinyama hivi vinaweza kujirudia mara kwa mara ni vizuri kuzingatia kujikinga na kupata maambukizi mapya.
Baadhi ya njia zinazotumika ni kupewa dawa ya kupaka ambayo inaviunguza vinyama hivi,au hata kuhitaji kufanyiwa upasuaji.
Madhara ya viuvimbe hivi (Warts) ni yapi?
Madhara ya viuvimbe hivi (Warts) ni yapi?
•Virusi hivi husababisha magonjwa ya saratani hivyo vinaweza kupelekea kupata saratani.
•Mama mjamzito aliye na ugonjwa huu anaweza kumuambukiza mtoto wake.


Tahadhari:
~Mwili hujaribu kupambana na virusi hivi na hivyo kuna baadhi ya watu ambao viuvimbe hivi huisha vyenyewe hata bila matibabu.
~Unaweza kupata kirusi hichi na usionyeshe dalili zozote hivyo ni vizuri kutumia kinga au kutembelea hospitali pale unapodhani humuamini mtu uliyejamiiana nae bila kinga.
~Dalili zinaweza kuchukua wiki, mwezi au hata miaka baada ya kukutana kimwili na mtu mwenye maambukizi haya.
Asante dokta naomba niongezee sababu mimi ni muhanga wa hili,kuna natural remedies za ugonjwa huu,,ambako unamia kitunguu swaumu kupaka juu ya zile warts zinapotea kabisa,lakini kama mpe wako ndo amekuambukiza ukijamiiana naye tena bila kinga vinarudi,,hivo ni vyema kuwa makini kwenye mahusiano yetu. Asanteni sana
Asante sana kwa ushauri🙏🏼
Asante kwa elimu nzuri dokta,je ukiwa na warts ndo unapata kansa ya mlango wa kizazi?
Hapana
Si lazima
Virusi hivi vina aina tofauti tofauti
Japo ni vyema kupima kipimo cha pap smear ili kuonyesha kama warts zimeleta mabadiliko yoyote katika tissue za shingo ya uzazi
Wow niliwahi kuona mahali kuwa kula vizuri na kunywa maji mengi,kupumzisha mwili kurelax kunaweza kukusaidia ukiwa na warts..
Asante daktari kwa elimu nzuri
Umeelezea kwamba maambukizi ya hizi warts ni kwa njia ya kugusana, inapotokea mwanaume ana hizo warts kwenye scrotum afu wakati wa kufanya mapenzi akawa anamgusa mpenzi wake na hizo scrotum. Kutumia kinga kutasaidiaje hapo maana kawaida condom haifiki hadi kwenye scrotum
Ahsante kwa swali
Ni vyema akatibiwe kwanza ndio muendelee na kujamiiana.
Somo zuri,Mungu awabariki muendelee kuelimisha jamii
Amina, Ahsante sana Evance
article nzuri
je njia kuu ya kupata warts ni kugusana kwa kujaamiana tu? kama vikitokea mdomoni, kugusana kwa wapenzi kunaezaleta maabukizi?
Leo nimekita hasa upande wa kina mama na maeneo ya sehemu za siri zao, ilakini hata ikiwa mdomoni inaambukizika kwa njia kama kupigana busu.
kwa nini watu hawaachi kujamiiana hovyo wakati magonjwa mengi hivi?
Habari.
Karibu DaktariMkononi.
Kujamiana kuna faida zake pia pamoja na kupata watoto.
Japo jamii inabidi watumie njia salama wakati wakujamiana kama matumizi ya kinga (kondomu).
Karibu.
habari, asanteni kwa ujumbe mzuri wa afya kwa jamii nilikuwa na wazo la kuboresha zaidi huduma hiyo. Kama inafaa tafadhali wasiliana nami kwa hii email
fictionaldesire9@gmail.com
Ahsante nimelielwa somo
Shukrani na karibu sana
Dokta nakupataje mie ni muhanga wa warts
Habari Azizi
Unaweza kumpata Daktari kwa kutumia namba zetu za simu
Unaweza piga simu au kutuma ujumbe mfupi.
0688 636 717
0762 952 137
Karibu