Shida ya kulala wakati wa ujauzito.

Tatizo la kushindwa kupata usingizi vizuri wakati wa ujauzito hutokana na sababu mbalimbali. Baadhi ya sababu hizo huweza kuwa kiungulia, mama kuhisi haja ndogo mara kwa mara, maumivu ya mgongo, misuli ya miguu kukaza,wengine pia huweza kuhisi kama madudu wanatembea miguuni ( restless leg syndrome) na kadhalika.
Hali hizi tajwa huokea kwa wajawazito wengi na zipo njia mbalimbali za kupunguza tatizo hili kulingana na shida mama anayoipata.

Huu ni  ushauri ambao unaweza kumsaidia mama mjamzito kupata usingizi mzuri hata wakati wa ujauzito.

•Mara baada ya kula, mama anashauriwa kuepuka mkao wowote wa kulala au kulala kabisa kwani huongeza uwezekano wa kupata kiungulia. Ikiwa tatizo linendelea, unaweza kujaribu kupunguza kiasi cha chakula unachokula wakati wa usiku. Jifunze zaidi kuhusu kiungulia kupitiahttp://daktarimkononi.com/2018/03/02/2332/

•Punguza au epuka vinywaji vyenye gesi kama vile soda ambavyo baadhi ya tafiti huonyesha kuwa zinaathiri upatikanaji wa madini ya Calcium mwilini hivyo huchangia katika kuleta tatizo la misuli kukaza. Mama anaweza kutumia vyakula vyenye madini hayo kama vile maziwa, mboga za majani.

• Mama hushauriwa kulala upande, hasa akilalia upande wa kushoto. Hii humsaidia kupunguza maumivu mgongoni na husaidia katika kuboresha mzuunguko wa damu. Unaweza kuweka mto laini katikati ya magoti, na chini ya tumbo.

•Punguza kutumia vimiminika wakati wa usiku, ili kutusaidia usiamke mara kwa mara kwenda haja ndogo.

• Fanya mazoezi kidogo ya kutembea jioni, na kula vyakula vyenye madini ya chuma na vitamini B-9 yaani folic acid. Vyakula hivi ni kama vile nyama, maini, samaki, mayai, maharage, parachichi, ndizi, papai vyote huweza kusaidia kuongeza virutubisho hivi mwilini hivyo kusaidia kupunguza restless leg syndrome

Furahia safari yako ya ujauzito. Usisite kuonana na mtaalamu wa afya pale uonapo dalili zozote katika ujauzito wako.

 

1 thought on “Shida ya kulala wakati wa ujauzito.

  1. Mtoto wangu amelalia ipande wa kulia mimi nni mjamzito miez 8 hvo inanifanya nishindwe kulala upande huo napia wakat wa usiku muda mwingine najikuta nipo upande wa kulia je siwez kumdhuru mtt kulala upande aliolala yeye?

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show