Matumizi ya dawa kwa mama kipindi cha kunyonyesha

Ni muhimu kwa mama wote wanaonyonyesha kuwaarifu madaktari wa watoto wao kuhusu kila dawa wanazotumia, ikiwemo dawa za asili (mitishamba). Sio kila dawa itakayotumika itapatikana kwa kiwango hatarishi katika maziwa ya mama na kusababisha madhara kwa mtoto. Kuna aina kadha wa kadha ya dawa ambayo huweza kusababisha madhara makubwa sana kwa watoto na nyingine kutokua na madhara kwa watoto na. Wakati huo huo, kuna dawa ambazo anaweza akapewa mama atumie ili aweze kutibu maradhi ya mtoto kwasababu zinakuwa katika mfumo wa vidonge ambapo mtoto hatoweza kutumia.

Dawa zisizo na athari ni zile za kupunguza maumivu, kuondoa wasiwasi (anti-depressants) na dawa za kutibu waathirika wa madawa ya kulevya, vileo na wavutaji wa sigara.

Kunyonyesha kwa mama hakuingiliani na chanjo ambazo mtoto hupata wakati wa kliniki na pia imegundulika kusaidia kupunguza homa azipatazo mtoto kutokana na chanjo hizo. Pia hutumika kama kinga asilia kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto .

Antibayotiki hupita kwenye maziwa ya mama kwa kiasi, hivyo kama mtoto ana uwezo wa kutumia dawa hizo basi dawa hizo hazina madhara kwa mama anaenyonyesha kuzitumia. Itambulike kua sio kila antibayotiki ni salama kwa mtoto.

Dawa kama Erythromycin hupatikana kwa kiwango kikubwa kwenye maziwa kuliko inavyoonekana kuwepo katika mfumo wa damu wa mama, dawa za kupunguza maumivu zimeonekana kua na athari ndogo kwa mtoto. Dawa zenye madini aina ya Salfa haziruhusiwi kupewa mama anaenyonyesha.

Kwa ujumla antibayotiki huruhusiwa kupewa mama anaenyonyesha endapo tuu dawa hio ni salama kwa mtoto.

Mambo ya kuzingatia mama anaenyonyesha.

  • Kutumia dawa kwa muda mrefu au zinazofanya kazi kwa muda mrefu.
  • Kutumia dawa mara tuu baada ya kunyonyesha (hii hutegemea na matumizi ya dawa hiyo).
  • Kua na ukaribu na mtoto na kua na tabia ya kuchunguza mabadiliko yoyote yanayo mtokea mtoto kipindi kizima utumiapo dawa hiyo.
  • Dawa nyingi zipatikanazo bila cheti cha daktari huwa na kemikali aina ya Ephedra ambayo sio rafiki kwa mtoto.
  • Zuia matumizi ya mchanganyiko wa dawa.

Athari za dawa kwa mtoto.

Kuathiriwa kwa mtoto hutegemeana na aina ya dawa, kiasi cha dawa (dozi) na njia ambayo dawa hiyo hunywewa.

Kuhara, kutapika na usingizi usio wa kawaida nk. ni athari chache anazoweza kupata mtoto. Dawa nyingine huweza kusababisha maziwa kuto kutoka kwa kiasi kinachotakiwa.

Mfano wa dawa hatari kipindi cha kunyonyesha ni kama dawa za aleji, dawa za kutibu saratani nk.

 

Ushauri kutoka kwa daktari unabidi uzingatiwe na inampasa mama kuzungumza na daktari juu ya mabadiliko yoyote atakayo yaona kutoka kwa mtoto wake. Kabla ya mama kutumia dawa ya aina yoyote kipindi cha kunyonyesha inampasa azungumze na daktari wake.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show