Muingiliano wa tunda la balungi na dawa

Balungi ni tunda ambalo wengi wanalipenda kutokana na ladha yake ya kipekee. Pamoja na hayo ni tunda ambalo lina kiasi kikubwa cha vitamin A na vitamin C , vitamin zinazohitajika katika kuimarisha kinga ya mwili, macho na ngozi.

Vile vile tunda hili linavirutubisho vya magnesium, calcium na potasium muhimu kwa afya.Tunda hili linauwezo wa kuingiliana na dawa mbali mbali mwilini kwa kuwa ni chanzo cha kemikali zinazoitwa furano coumarins zinazoingiliana na mfumo wa mwili wa kumeng’enyua dawa. Muingiliano huu husababisha ulimbikizaji wa dawa mwilini, hali ambayo husababisha athari mbali mbali kwa mgonjwa kulingana na dawa. Dawa zinazoingiliana na tunda hili kwa njia hii ni kama dawa za magonjwa ya moyo(mf. amiodarone), dawa za kupunguza mafuta mwilini (mf. Simvastatin) n.k. Tunda moja au juisi kiasi cha 200mls inatosha kusababisha muingiliano huu. Hivyo kwa wapenzi wa tunda hili inashauriwa kumuuliza mfamasia kila unapopewa dawa kiasi cha tunda hili au juisi unayoweza kunywa wakati wa matibabu. Japo mara nyingi inashauriwa kutokula hili tunda wala juisi yake mpaka pale matibabu yanapokamilika.
Balungi ni tunda ambalo lipo katika familia ya citrus hivyo matunda mengine ya familia hiyo kama aina fulani ya machungwa na ndimu huweza pia kuwa na muingiliano na dawa japo ni kwa kiasi kidogo zaidi.

Privacy Preference Center