Harufu mbaya ukeni; ungependa kujua chanzo!?

Wanawake wengi hujiamini pale wanapokua na uke usiokuwa na harufu au ute tofauti na ule waliozoea. Mara moja moja hali hii huweza kubadilika kutokana na sababu mbalimbali hata kama unajitahidi kuutunza uke wako vizuri kabisa. Hali huwa siyo ya kawaida endapo mabadiliko haya yatadumu kwa muda mrefu au harufu itakua kali sana.

Kwanza kabisa inakupasa kutambua harufu ya kawaida ya uke; harufu hii huwa ni asilia na hutofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine. Katika hali ya kawaida uke wenye afya huwa na harufu ya nyama mbichi. Kuwa kwenye hedhi au kufanya mapenzi kunaweza kubadilisha harufu hii kwa muda mchache.

Harufu mbaya ya uke huweza kuambatana na kutokwa na ute wenye hali ya tofauti pia aidha katika rangi au uthabiti ukiguswa na vidole (consistency). Kawaida ute kutoka kwenye uke huwa ni kama maji maji yasiyo na rangi ambao huwa na hali ya kuvutika wakati yai linatoka kwenye ovari (ovulation).

Tofauti katika rangi huweza kuwa;

  • Nyeupe: huweza kuwa hali ya kawaida mwanzoni au mwishoni mwa hedhi lakini inapoambatana na muwasho na kuwa na muonekano wa jibini huashiria maambukizi ya fangasi.
  • Kahawia (brown) au enye damu (bloody): hii ni hali ya kawaida unapokua kwenye hedhi na unapomaliza huweza kuwa na muonekano wa kahawia. Ikitokea ukapata matone katikati ya mzunguko wa hedhi huweza kuashiria mimba au dalili ya saratani ya shingo ya kizazi.
  • Njano au kijani: hasa ute ukiwa pia mzito na wenye harufu mbaya (wakati mwingine harufu ya samaki) huwa ni ishara ya maambukizi ya vimelea kama bakteria na protozoa. Mtu huvipata vimelea hivi kwa njia ya kufanya mapenzi.

Kuepukana na tatizo hili

  1. Jiweke safi kwa kuzingatia njia sahihi za kusafisha uke wako kama ilivoelezewa kwenye makala ya kusafisha uke.
  2. Badili aina ya nguo ya ndani unayovaa endapo haijatengenezwa kwa pamba kwani pamba ina uwezo mkubwa wa kufyonza unyevunyevu na kukuacha mkavu.
  3. Pendelea kunywa mtindi kwani huweka mazingira ya uke wako kuwa na hali nzuri na yenye afya.

Muone daktari kwa ajili ya matibabu sahihi mara tu hali ya harufu yako itadumu kwa muda mrefu, itazidi kuwa kali siku zinavoenda au itaambatana na ute usio wa kawaida.

4 thoughts on “Harufu mbaya ukeni; ungependa kujua chanzo!?

  1. Asante dokta,,tunaomba mtueleze vizuri faida za chupi za cotton na blazia pia,,na je ni sahihi kuvaa vya mtumba?!

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show