Harufu mbaya ya kwapa


Jasho ni moja ya njia maalumu ya mwili ya kurekebisha kiwango cha joto la mwili, ila inapofika wakati jasho hili linaanza kutoa harufu mbaya hua kero kwa mtu anaetoa harufu na kwa jamii nzima inayomzunguka.

Kwa kawaida jasho hua halina harufu, kwani jasho ni mchanganyiko wa maji na aina mbali mbali za madini chumvi yanayotolewa kama taka mwili,

Harufu mbaya ya kwapa husababishwa baada ya bakteria kumeng`enya aina flani ya protini inayozalishwa pamoja na jasho kutoka katoka tezi maalumu za jasho ziitwazo apocrine glands. Tezi hizi zinapatikana katika maeneo ya makwapa, matiti, maeneo ya sehemu za siri na katika kope za macho.

Kwa baadhi ya watu hali hii ya kunuka kwapa hua sugu sana na hivyo kua kero kwao na jamii kwa ujumla. Ili kupunguza harufu au kuimaliza kabisa yapaswa kupunguza pia kiwango cha jasho unalozalisha kwa siku kwa kufanya yafuatayo;

1; Kula mlo kamili na fanya mazoezi ili kupunguza mwili, kwa sababu watu wanene huathiriwa sana na tatizo hili kwa sababu ya mikunjo mikunjo ya ngozi yao hivyo kutoruhusu jasho kukauka mwilini.
2; Vaa nguo za pamba , nguo za aina hii husharabu jasho la mwili na kukuacha mkavu, epuka pia nguo zanazokubana sana.
3; Tumia manukato mbalimbali ili kupambana na harufu.. pia tumia dawa maalumu zinazoweza kupunguza kiwango cha jasho linalizalishwa kwenye makwapa (muone daktari wako kwa kupata dawa hizi)
4;Kua na tabia ya kuoga mara kwa mara.. kila unapokua umefanya shughuli yoyote ya kukutoa jasho, ni vizuri kutumia medicated soap ili kuua bakteria wanaozalisha harufu mbaya.
5;Epuka vyakula na vinywaji vinakavyokufanya utoe jasho. Vyakula kama pilipili, kahawa, pombe, vitunguu;
6;Nyoa nywele za kwapani. Kwa sababu uepo wa nywele hizi husababisha jasho kutokauka.. hivyo bacteria kuzalisha harufu kutokana na jasho hili.
7; Kula mboga mboga za majani kwa wingi husaidia kupunguza kiwango cha jasho mwilini
8;Kunywa maji ya kutosha kila siku.
9;Badilisha nguo kila siku.. ili kupunguza mrundikano wa jasho.
10;Punguza msongo wa mawazo kwa kufanya vitu vitakavyokupa burudani kama kusikiliza muziki na mengineyo, hali hii hupunguza kiwango cha jasho mwilini.

Muone daktari wako endapo una matatizo yafuatayo;
1; unatoka jasho kwa wingi wakati wa usiku mpaka unalowanisha nguo au shuka zako
2;unatokwa na jasho nyingi kuliko kawaida ulivyozoea
3;unatoka jasho kipindi cha baridi
4;jasho lina kunyima uhuru wa kufanya kazi zako za kila siku.

1 thought on “Harufu mbaya ya kwapa

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show