Matibabu ya mzizi wa jino(root canal treatment)

Hii ni aina ya matibabu ya jino ambapo sehemu hai ya jino(pulp tissue)iliyoshambuliwa na kuharibiwa na  bakteria  inatolewa na mizizi ya jino kusafishwa vizuri kisha kujazwa kwa  material maalum.

Matibabu haya hutolewa kwa jino ambalo limeharibika kiasi kwamba haliwezi kutibika kwa kuziba kawaida  tu na matibabu haya yanaweza kufanyika kwa siku moja kwa baadhi ya meno na mengine zaidi ya siku moja.Watu wengi kwenye jamii yetu bado hawajajua kuhusu matibabu haya na hivyo kukimbilia kung’oa meno yao pale maumivu yanapokuwa makali sana.

Sababu za kufanya matibabu ya mzizi wa jino(indications)

 • Jino lililotoboka kiasi cha kushindwa kuzibika kwa njia ya kawaida
 • Jino kuvunjika hadi kwenye kiini kutokana na ajali au kuanguka.
 • Maandalizi ya kuwekewa aina fulani ya meno bandia(crowns and bridges)
 • Kuharibika kabisa kwa mzizi wa jino(pulp necrosis)

Sababu ambazo zinafanya matibabu haya yasifanyike(contraindications)

 • Meno yaliyoharibika sana ambayo hayawezi kutibiwa tena pamoja na yale yaliyovunjika vibaya kwenye mzizi(vertical tooth fracture)
 • Meno amabayo hayajashikiliwa vizuri kwenye taya(lack of periodontal support)
 • Meno ya wagonjwa ambao hawana ushirikiano mzuri mf watu wenye matatizo ya akili
 • Sehemu yenye saratani au uvimbe
 • Meno ya wagonjwa wenye afya mbaya ya kinywa na meno amabayo haiwezi kurekebishika kwa mda huo

Matibabu ya mzizi wa jino huanza pale tu ambapo x-ray imeweza kudhibitisha kuwa kiini cha jino kimeshambuliwa na vijidudu(bacteria) au kimeguswa na kuvunjika kwa jino husika.

Kinachofanyika wakati wa matibabu haya ni:

 • Mgonjwa anachomwa sindano ya ganzi katika hilo eneo ambapo jino lipo ili kuzuia maumivu wakati wa matibabu
 • Sehemu ya ndani ya jino inasafishwa vizuri mpaka kwenye mizizi na kisha xray ya ilo jino inachukuliwa ili kuhakikisha kwamba mizizi yote imefikiwa na kusafishwa vizuri
 • Jino sasa litajazwa vizuri,kama halitahitaji mahudhurio mengine basi litajazwa moja kwa moja(permanent filling)
 • Kama jino litahitaji mahudhurio zaidi ya mara moja basi litajazwa kwa material ambayo sio ya moja kwa moja(temporary filling)

  kabla na baada ya matibabu ya mzizi wa jino

Matibabu yanapokamilika mgonjwa anaweza sasa kutumia  jino lake vizuri tu kama kawaida ila cha kuzingatia ni afya nzuri ya kinywa ili jino hilo lidumu na pia kuzuia meno mengine kutoboka.Maumivu yakiendelea baada ya matibabu rudi kwa uchunguzi zaidi.

 

 

 

 

7 thoughts on “Matibabu ya mzizi wa jino(root canal treatment)

 1. Asante dokta kwa maelezo mazuri,eti kwa jino ambalo limebakia mzizi naweza kufanya haya matibabu na kuwekewa jino bandia au lazima ning’oe?

  1. Swali zuri Maria,inategemea na kiasi gani cha kimebakia,kuna baadhi ya meno hasa ya mbele mzizi unaweza kusafishwa na mtu kuwekewa crown,kuna changamoto kwenye meno ya nyuma lakini.Hivo ni vema kuwahi matibabu mapema na kujenga utaratibu wa kuchunguzwa kinywa na meno yako.

  1. Mara nyingi hutokea kama jino halikusafishwa vizuri wakati wa matibabu hivo kutokea kwa maambukizi ndani ya jino,,pia inawezekana baadhi ya material yanayotumika kuleta mabadiliko ya rangi.Ukiona jino linaanzakubadilika fika hospitali kupata msaada.

 2. Daktari jmn mm nina meno yamezibwa lakini cha kushangaxa yananiuma vibaya sana jamani na nina mengine mengi yanaashiria kuanza kuoza.
  Nafanyaje maana inaelekea kuziba huwa sio permanent, maana naona yanabomoka.. nisaidie nateseka vibaya mno

  1. Pole Elica,tiba pekee ya jino lililotoboka ni kuziba,na kuzuia meno mengine kutoboka ni kwa kupunguza matumizi ya vyakula vya sukari hasa katikati ya mlo mmoja na mwingine,,vyakula kama juisi,soda,pipi,biskuti na aina nyingine za sukari,,pia tumia dawa ya mswaki yenye madini ya floridi itakusaidia kupunguza meno kutoboka,,
   kwa hayo meno yanayouma nenda tena hosptali kwa uchunguzi zaidi na matibabu usibaki na maumivu.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show