Sababu za vipele kuota sehemu za siri baada ya kunyoa

Watu wengi Waume kwa wanawake hukoseshwa raha na matatizo mengi ya sehemu za siri. Moja wapo ya tatizo hili ni kutokewa na vipele baada ya kunyoa nywele huotazo sehemu hizo.

Nini Umuhimu wa hizo nywele sehemu za Siri ?

● Nywele za uke na uume huzuia maambukizi ya bakteria ambao huweza kupenya kwenye vitundu vidogo vya sehemu hizo,vilevile huzuia mchubuko wa ngozi katika sehemu hizo.

● Sababu hii haimaanishi usinyoe  sehemu za Siri. Sehem hizi zikizidi nywele hutoa harufu mbaya. Hivyo zingatia husafi na unadhifu pia.

Nini kinasababisha vipele hvi?

Sababu zipo nyingi. Baadhi ambazo ni sababu kwa wengi ni kama:

● Urudiaji wa kiwembe ulichokwisha kukitumia uliponyoa kabla ya siku hiyo au kutumia kiwembe butu kama njia ya kunyolea.
● Kunyoa uelekeo tofauti na nywele zako zinavyoota.

Nini nifanye baada ya kupata vipele?

Mara nyingi vipele hivi hupotea vyenyewe baada ya muda, Ila kuna vingine huwepo kwa muda mrefu na hata kuanza kuuma na kutengeneza usaha. Baadhi ya njia husaidia ni kama:

● Kutumia kitambaa safi na maji ya vuguvugu kukanda sehemu iliyo na tatizo hilo.
● Matumizi ya asali na maji ya vuguvugu pia husaidia kupunguza vimelea vya bakteria wowote katika eneo hilo na hupunguza vipele hivyo
● Matumizi ya yai. Yai linaprotini ziitwazo albumin ambazo husaidia sana ngozi.kwahyo husaidia kuponesha ngozi yenye vidonda au vipele kwa haraka.unatumia sehemu ya nje (nyeupe) ya yai kupaka sehemu husika unaacha inakaukia hapo halafu unabandua,inatoka pamoja na kipele hasa kilichoanza kutunga usaha.
● Matumizi ya sukari kama scrub. Sukari ina glycolic acid ambayo hupenya kwenye ngozi na kusaidia kuua seli zilizokufa na kuponya ngozi iliyoharibika eneo hilo haraka. Jinsi ya kutumia?Changanya sukari na mafuta ya olive kama unayo, kama huna tumia ata ya nazi kisha paka sehemu husika na sugua taratibu kwa kuzungusha taratibu kuelekea juu kisha acha kwa muda. Alafu toa kwa maji ya vuguvugu. Rudia hivi hadi vitakavyokwisha.
Endapo njia hizi hazikusaidii, muone daktari wa ngozi kwa matibabu sahihi zaidi.

Nini nifanye kuzuia vipele hivi?
● Kwanza tumia maji ya vuguvugu ulowanishe sehemu hiyo unayonyoa, kisha tumia sabuni/shaver cream kuweka povu la kutosha ili unyoe kirahisi zaidi kwa maana nywele zinaasili ya kuota kwa kujifungafunga na ni ngumu pia, hivyo kwa kulainisha hupunguza uwezekano wa kupata vipele.
● Baada ya kulainisha nyoa kwa kutumia kiwembe/mashine ya kunyolea mpya kwa uwelekeo ambao nywele zako huota.
● Baada ya kunyoa ni vyema kutumia aftershave ambayo husaidia kuzuia bakteria ambao wanaweza kupenya kwenye vitundu vidogo baada ya kunyoa
● Vilevile imeelezwa kuwa hupaswi kunyoa nywele zote za uke au uume na kuacha kipara, kwasababu huongeza hatari za magonjwa ya ngono wakati wa tendo la ndoa majimaji na bakteria huweza kupenya kutokana na vitundu vidogo vinavyokuwepo baada kunyoa nywele zote.

Muone daktari endapo hali hii haiishi na haswa vipele vikiendelea kutokea, vinatoa usaa, vinauma sana na vinakuwa vyekundu.

4 thoughts on “Sababu za vipele kuota sehemu za siri baada ya kunyoa

  1. Asante,,sasa nitawezaje kunyoa na kuacha nywele yaani kutokuweka kipara kama unavoshauri kwa kutumia hz sheva zetu?

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show