Weusi katikati ya mapaja; nini sababu hasa!?

Mtu yeyote anaweza kupata weusi katikati ya mapaja bila kujali rangi ya ngozi yake. Hali hii husababishwa na mlundikano wa ngozi iliyokufa au ngozi kutengeneza kiasi kikubwa cha melanin ambayo kawaida kazi yake huwa ni kuipa ngozi yako rangi uliyonayo.

Mabadiliko haya ya ngozi yanaweza kufika mpaka kwenye eneo linapopita mistari ya chupi.

Sababu za hali hii
Kuna sababu mbalimbali zinazopelekea mtu kuwa na tatizo hili, baadhi ya hizo ni:

 • Maumivu yanayotokea katikati ya mapaja wakati wa kutembea au kufanya mazoezi ngozi inaposuguana. Hii hupelekea ngozi kuwa nyembamba, yenye muwasho na nyeusi zaidi.
 • Mabadiliko katika homoni mtu anapokua ananyonyesha, akiwa na mimba au kwenye hedhi na pia magonjwa kama ‘Polycystic ovarian syndrome (PCOS)’.
 • Baadhi ya dawa mfano vidonge vya uzazi wa mpango na baadhi dawa za matibabu ya saratani.
 • Ngozi kuangazwa na jua kwa muda mrefu na kuwa na ukavu wa ngozi.
 • Msuguano wa ngozi na nguo zinazobana.
 • Magonjwa kama kisukari, pumu ya ngozi na ‘Acanthosis nigricans’.

Upatapo tatizo hili unaweza kuonana na daktari wa ngozi kwa ajili ya ushauri na matibabu sahihi.

Ukiwa mwenyewe nyumbani unaweza kujaribu njia zifuatazo;

 1. Mchanganyiko wa mafuta ya nazi na limao: mafuta ya nazi hufanya ngozi kuwa nyororo huku limao likiwa na vitamin C yenye uwezo wa kuondoa weusi huo. Changanya vijiko kadhaa vya mafuta ya nazi na juisi ya limao uliyoikamua kutoka kwenye kipande kimoja cha limao. Sugua eneo lililoathirika kwa dakika 10 kisha safisha na maji.
 2. Mchanganyiko wa limao, sukari na asali: sukari inauwezo wa kuondoa ngozi endapo kuna mlundikano wa ngozi iliyokufa. Changanya juisi ya limao, sukari ujazo wa kijiko cha chai na asali ujazo wa kijiko cha chakula. Sugua kwenye weusi na baada ya muda safisha na maji.
 3. Aloe vera: huu ni mmema unaojulikana na wengi na una uwezo mkubwa wa kutakatisha ngozi. Unaweza kutumia ute wa mmea wenyewe au bidhaa ziliyotengenezwa na aloe vera. Paka kama mafuta kwenye eneo lenye weusi na uache dawa ipenye, huhitaji kuosha na maji baada ya kupaka.
 4. Viazi mviringo: hivi vina uwezo pia wa kuondoa weusi. Kata kipande cha kiazi na usugue eneo lililoathirika kwa walau dakika 15 kisha safisha na maji.

Jinsi ya kuzuia hali hii

 • Zuia msuguano wa ngozi kwa kuvaa nguo za ndani kama stockings na skintights
 • Safisha vizuri katikati ya mapaja yako kuzuia mlundikano wa ngozi iliyokufa.
 • Epuka kuvaa nguo zinazobana zitazokuletea kutoka jasho na msuguano.
 • Linda ngozi yako kwa kuepuka kuiangaza kwenye jua kwa muda mrefu.

17 thoughts on “Weusi katikati ya mapaja; nini sababu hasa!?

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show