Madhara ya kutumia vidonge vya kutuliza maumivu kiholela (NSAIDs).

       kumekuwa na utaratibu ambao umekuwa wa kawaida sana katika jamii yetu ya kitanzania kuhusiana na matumizi ya kiholela ya dawa za kutuliza maumivu yani NSAIDs.

”   Dawa hizi zimekuwa zikitumiwa kwa ajili ya kutuliza maumivu ya sehemu mbali mbali katika mwili mfano, maumivu ya kichwa, maumivu ya mifupa, yani mgongo, mifupa (joints) lakini pia maumivu makali wakati wa hedhi (Dysmenorrhea) dawa hizi hutumika kutuliza maumivu kwa wanawake.

Mfano wa dawa hizo za maumivu zinazojulikana na watanzania wengi ni kama Diclofec, Ibuprofen (brufen), mefenamic acid (Meftal), Indomethacin (wengi hutumia kama dawa ya kuulia panya), ketoprofen naproxen, pamoja na celecoxib. Pamoja na uwezo mkubwa wa dawa hizi kutuliza maumivu dawa hizi huweza kuleta matatizo mengine mengi kama zisipotumiwa kisawa sawa kama ilivyo elekezwa na mhudumu wa afya.

 Yafuatayo ni madhara ya matumizi ya kiholela na kwa muda mrefu ya dawa hizi za kutuliza maumivu kwa zaidi ya siku 45 (NSAIDs)

 1. Husababisha maendeleo mabaya ya vidonda vya tumbo wakati mwingine kuvuja damu tumboni (Gastric ulcers).
 2. Uwezekano wa kupata magonjwa ya figo (Acute kidney injury) kwa sababu dawa hizi hupunguza kiasi cha damu kinachoenda kwenye figo kwa ajili ya kusafishwa (Hii huwapata mara nyingi watumiaji wa dawa hizi kwa zaidi ya siku 45).(Renal-hypoperfusion).
 3. Pia dawa hizi huzuia uwezo wa mwili kugandisha damu iwapo mtumiaji atapata jeraha (bleeding tendecy).
 4. Magonjwa ya moyo na shinikizo la damu lenye uhusiano na kuharibika kwa figo (RAAS activation).

Je ni nini unatakiwa kufanya ili kujiepusha na madhara haya?

 1. kuachana na matumizi ya dawa hizi (NSAIDs) bila ushauri wa mhudumu wa afya ni njia ya kwanza ya msingi kwa mtumiaji.
 2. kutumia dawa za maumivu za aina moja bila kubadilisha badilisha sana dawa hizi mfano diclofenac au Sulindac.
 3. kutumia kiasi cha dozi cha dawa kama ilivyo elekezwa na mhudumu wa afya.
 4. Endapo dawa hizi za maumivu hazijakusaidia ni vyema ukaonana na daktari.

3 thoughts on “Madhara ya kutumia vidonge vya kutuliza maumivu kiholela (NSAIDs).

 1. Asante daktari kwa elimu nzuri
  Hizo siku 45 ni mfululizo au zinahesabiwaje!? Na kubadilisha Badilisha dawa za maumivu kunaleta athari gani

Leave a Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.

Top Posts & Pages

Recent Comments

CATEGORIES

Ratiba ya Wiki Hii

Jumatatu: Afya ya mtoto
Jumanne: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Jumatano: Magonjwa ya Dharura na Magonjwa mengine
Alhamisi: Lishe na Mazoezi
Ijumaa: Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake
Jumamosi: Afya ya uzazi
Jumapili: Magonjwa ya kuambukiza

POST REVIEWERS

Afya ya mtoto: Dr. Julieth Joseph
Afya ya Kinywa na Meno: Dr. Baraka Kileo
Famasia: Pharm. Hans Nniko
Sexual Health Dr. Deogratius Mtei
Lishe na Mazoezi: Dr. James Hellar
Magonjwa ya Dharura: Dr. Kilalo Mjema
Magonjwa ya moyo na Shinikizo la damu: Dr Hussein Manji
Saratani: Dr. Mathew Cosmas
Ujauzito na Magonjwa ya Wanawake: Dr. Walter Msirikale

About Us

Daktari Mkononi is a platform that contains health related information and connects health personnels and the society. Made by a group of medical students and overseen by doctors with love and passion to ensure healthy lives 🙂

CONTACT

Email:
daktarimkononi@gmail.com

SMS:
+255684159117
+255768256424

Whatsapp:
+255688636717

Subscribe

Tuandikie email yako tukutumie mada mbali mbali za afya uzipendazo.

Recent Posts

Upcoming Event

Homa ya Kichaa cha Mbwa | 28th September

Upcoming Show